Monday, December 21, 2015

CCM YAIBUKA KIDEDEA KITI CHA UBUNGE JIMBO LA MASASI MKOANI MTWARA.BOFYA HAPA






Msimamizi  wa  uchaguzi   Jimbo  la  Masasi  Mkoani  Mtwara  FORTUNATUS  KAGORO  amemtangaza  rasmi  CHUACHUA  RASHID     wa CCM kuwa mbunge  baada  ya  kupata  kura  kupata  kura  16597 dhidi  ya  mpinzani  wake  wa   karibu ISMAIL  MAKOMBE  maarufu  kama KUNDAMBANDA  wa  CUF  aliyepata  kura  14069 KATIKA  Uchaguzi  mdogo  uliofanyika  Desemba  20  kutokana  na  kifo  cha  aliyekuwa  mgombea  ubunge  jimbo  hilo Dk  Emmanueli  Makaidi  wa  NLD

Wakala  wa  majumuisho  wa CUF Maftaha  Nachumba  ambaye  ni  mbunge  wa  jimbo  la  Mtwara  mjini  amekubali  matokeo  na  kusema  kuwa  tofauti  iliyojitokeza  ni  ndogo  lakini  kilichowaangusha  zaidi  ni  mwitikio  mdogo  wa  wananchi  waliojitokeza  kupiga  kura.

 Kaimu  Katibu  wa  CCM wilaya  ya Masasi   Ajali Mussa  amesema  mikakati  na  sera  za  chama  chake  ndiyo  ilikuwa  siraha  ya  ushindi  wao  Huku  mshindi  wa  ubunge  Chuachua  Rashid    akisema  ilani  ya CCM iligusa  maslahi  ya  wananchi  ndiyo  maana  wamewaamini  kuwachagua.

No comments:

Post a Comment