Wajumbe wa
mabaraza ya Kata
wametakiwa kuzingatia haki
na uzalendo katika
kutoa suluhu na
hukumu zao wanaposikiliza kesi
mbalimbali zinazofikishwa kwao
na wananchi wanaowazunguka kwasababu
haki huinua nchi
na uzalendo ni vitendo na
siyo maneno.
Wito huo
umetolewa na mwanasheria
wa halmashauri ya
Kyerwa Jovin Rutainulwa katika mafunzo
ya siku moja
ya kuwezesha mabaraza
ya kata wilayani
Kyerwa yaliyofanyika kwenye
ukumbi wa Western
Hotel amesema kuwa
wasipotenda haki na kuwa
wazalendo wanaweza kusababisha
malalamiko mengi kutoka
kwa jamii na wafanye
kazi hiyo kwa
uzalendo mkubwa.
Amesema kuwa anatabua kazi
kubwa waliyonayo pia
changamoto nyingi zinazowakabili wajumbe
wa mabaraza hayo
zikiwemo za ukosefu
wa vitendea kazi
na sehemu za
kufanyia kazi lakini
hicho kisiwe kigezo
cha kutotoa haki
kwa muda muafaka
na kushindwa kuwasaidia
wananchi waliowaamini kuwachagua.



No comments:
Post a Comment