Jeshi la polisi Kanda Maalumu la Dar es salaam linawashikilia askari sita kwa tuhuma za kusababisha vifo vya watu wawili waliotuhumiwa kujihusisha na vitendo vya ujangili.
Jeshi hilo linamtafuta Kachero wa polisi mwenye namba E 5371 Issa Kazimoto ambaye alitoroka mara baada ya kutokea kwa tukio hilo.
Kamishana wa Jeshi la Polisi Kanda Maalumu ya Dar es Salaam Suleiman Kova amesema miongoni mwa askari hao wawili wanatoka jeshi la Polisi na Wanne ni wa Idara ya Wanyama pori kikosi kazi cha kuzuia ujangili Tanzania.
Kova amewataja askari hao kuwa ni Mkaguzi wa Polisi Boni Mbage na askari mwenye namba E 919D/SGT Filbert maarufu kama Fulu saba na wa Idara ya wanyamapori ni Emmanueli Mbaga, Deogratius Mwageni,Joseph Jimmy na Asubile Mwakyusa
Amesema askari hao kwa pamoja wanadaiwa kufanya mauaji ya wakazi wawili wa jijini Dar es Salaam ambao ni Yasini Rashind mwenye miaka 46 mkazi wa Mabibo na Samson Masigare mwenye umri wa miaka 46 maarufu kama Ngosha mkazi wa Mbezi tukio hilo lilitokea Desemba 19 mwaka huu.


No comments:
Post a Comment