Mwenyekiti wa kitongoji cha Malulu Saimon Mgacha na Kaimu afisa mtendaji wa kijiji hicho Mwita Mseti wamemtaja aliyekamatwa ni Ntare Nyambane Ntare mwenye umri wa miaka 30
Baada ya Mashauriano yaliyofanyika ofisi ya kijiji hicho yaliyohusisha mmiliki wa Mbuzi huyo Mwita Chongo wamesema kitendo kilichofanywa na mtuhumiwa huyo ni kibaya na cha aibu kwa jamii hivyo wakaamua kumpatia adhabu ya kuchimba shimo la choo lenye urefu wa futi 12 pamoja na kufanya usafi kwenye ofisi ya kijiji kwa kipindi cha miezi mitatu.
Katika utetezi wake mtuhumiwa huyo Ntare Nyambane Ntare amesema anaomba msamaha na hajui kilichomtokea mpaka kutenda tukio hilo la ajabu kwani anaye mke na watoto na kukubali kutimiza adhabu aliyopewa na viongozi hao.


Dah! Hatari sana
ReplyDeleteduh! balaa!
ReplyDelete