Mwenyekiti wa
Kikao cha uchaguzi
wa kumpata mwenyekiti
wa halmashauri ya
Kyerwa Godian
Rugaimukamu amekataa kutii zuio
la mahakama ya hakimu
mkazi Bukoba la
kuwakataza kutoendelea na
zoezi la uchaguzi
mpaka shauri lililofunguliwa na
chama cha Demokrasia na
Maendeleo (CHADEMA) kuhusu
mgawanyo wa viti
maalumu vya udiwani.
Akizungumza
baada ya zoezi
la kuapishwa kwa
madiwani wa halmashauri
hiyo Mgombea uenyekiti
aliyekuwa amesimamishwa na
CHADEMA Prudence Mweyunge
alisema kikao cha
kumchagua mwenyekiti siyo
halali kwasababu ya
kuwepo Zuio la
Mahakama mpaka shauri
lililofunguliwa na kupinga
kupewa viti maalumu
vya udiwani kinyume
na kanuni na
sheria zilivyo kwani
wao katika uchaguzi
walipata madiwani 13 na CCM
kupata madiwani 11 lakini mgawanyo
wa viti hivyo vilibadilika
ambapo chadema walipata
viti maalumu 4 na CCM
kupewa 5
Baada ya kutoa
maelezo hayo mwenyekiti
wa kikao cha
uchaguzi Godian Rugaimukamu
alikataa kutii Zuio
hilo la Mahakama
kwa sababu alizotoa kuwa
halikuwasilishwa kwa utaratibu
unaotakiwa kwani serikali
inao utaratibu wa kupokea
taarifa kwa maandishi na
badala yake nakala
ya Zuio hilo alikuwa
nayo diwani wa
kata Businde ambaye
alikuwa mgombea wa nafasi
ya uenyekiti kupitia
CHADEMA hata hivyo
hakushiriki zoezi hilo
la uchaguzi.
Madiwani wote
15 walioapa jana wa CHADEMA
baada ya kukataliwa
kwa hoja hiyo
waliamua kutoka nje
ya ukumbi na
kuwaacha madiwani wa
CCM pekee yao
ambao jumla yao
walikuwa ni 17
akiwemo na mbunge
wa jimbo la
Kyerwa wakaendelea na
kikao cha uchaguzi
wa kumpata mwenyekiti
wa halmashauri huku
ulinzi ukiwa umeimarishwa
na jeshi la
polisi kikosi cha
kutuliza ghasia hata
waandishi hawakuruhusiwa kuingia
ukumbini humo.
Katika
uchaguzi huo uliokuwa
wa upande mmoja
waliochaguliwa ni Kashunju Lunyogote
diwani wa Kata ya Rukulaijo
kwa nafasi ya
Mwenyekiti na makamu
mwenyekiti alichaguliwa Jonas
Vedasto wa Kata
ya Kamuli ambao
wote kwa pamoja
walichaguliwa kwa kura
18 za madiwani wa CCM waliopiga
kura hakuna iliyoharibika
hata moja.
Mwenyekiti
wa Chama cha
Demokrasia na Maendeleo
CHADEMA wilaya ya
Kyerwa Deus Rutakyamirwa akizungumza na
waandishi wa habari
mara ya kutoka
nje ya ukumbi
alisema kinachofanyika ni
hujuma za kuitaka
halmashauri kwa nguvu
waliopoona wamezidiwa kwa
nguvu za wananchi
kwa kuwachagua madiwani wengi.
Alisema
kuwa hujuma hizo
zilianzia kwenye nafasi
za viti maalumu
kwani wao walipata
madiwani 13 wakapewa
viti 4 na CCM
waliopata viti 11 walipewa
viti 5 alieleza
hiyo ni kinyume
na Kanuni na
sheria za kuwapata
madiwani viti Maalumu
hivyo wakaamua kufungua
shauri mahakama hakimu
mkazi Bukoba na
tayari sumansi ya
kuwaita mahakamani msimamizi
wa uchaguzi ngazi
ya jimbo ,mwanasheria mkuu
wa serikali (AG)na
mkurugenzi wa uchuguzi wa
tume ya Taifa wanatakiwa kuhudhuria
mahakamani Tarehe 14
mwezi huu ili kutoa
ufafanuzi huo wa
kisheria na ndiyo
maana wanashangaa Zuio
la Mahakamani Kutupiliwa
mbali.
Pia alisema
mleta Zuio hilo
alifuata utaratibu wote
ambapo siku ya
tarehe 09 ambayo ilikuwa
mapumziko alifika ofisi
za halmashauri na
kusaini kitabu cha Mlinzi
na siku ya
kikao ambayo ilikuwa
juzi(Jana) alifika asubuhi saa
moja na kusaini
kitabu alipoulizia wahusika
aliambiwa hawapo maeneo hayo
lakini taratibu zote
alisema kuwa ni
ukaidi wao tu.
Rutakyamirwa
alisema hujuma nyingine
ya kuitaka Halmashauri
ya Kyerwa ilikuwa
ni kupitia njia
ya kuwabambikizia kesi
ambapo diwani Mteule
wa Kata ya
Bugomora ambaye pia
ni Katibu Mwenezi
wa CHADEMA wilaya
Tulakila Libenti anashikiliwa
kwa tuhuma za
kuhusika na mauaji
huku diwani Mteule
wa kata ya
Kikukuru Eustace Rwegosora
aliondolewa kwenye kikao
muda mfupi kabla
ya zoezi ya
kuapishwa kwa madai
kuwa anatakiwa mahakamani
kwa kukabiliwa na
kesi ya kupiga
kura mara mbili.
“Kweli
ndugu waandishi hii inachekesha sana
diwani wetu Eustace Rwegosora
alishikiliwa siku ya
jumatatu ya tarehe
7 ya mwezi
huu mara baada
ya kuhairishwa ghafla
kikao ambacho walikuwa
waapishwe kwa madai
eti alipiga kura
mara mbili walimtoa
ofisini kwangu na
Jumanne ya tarehe
8 alipelekwa mahakamani
dhamana ikawa wazi
tukamdhamini alipotoka nje ya mahakama
alikamatwa tena na
polisi kwa madai eti
ni mhamiaji haramu
alipelekwa uhamiaji mkoa
na baadae kuachiwa sasa mnaona
maagizo hayo?”Alihoji Rutakyamirwa.
Mwenyekiti
huyo akizungumzia diwani
wa Bugomora Tulakila
Libenti alisema wakati
tukio la mauaji
likitokea katani kwake
yeye hakuwepo na
alikuwa wilayani kwasababu aliamua kukaa
huko kutokana na
vurugu zilizojitokeza Oktoba
15 wakai wa
Kampeini ambapo yeye
mali zake ziliharibiwa
ambazo ni magari
matatu, pikipiki
mbili,Saluni ya kunyoa
nywere ambayo ilikuwa
inatumika pia kama
ofisi ya chama
katani humo pamoja
na mali kadhaa
za wafuasi wa
CHADEMA akiwemo baba yake
mzazi.
Akizungumza
mara baada ya
kuhairishwa kikao Makamu
mwenyekiti wa halmashauri
aliyechaguliwa Jonas Vedasto
alisema kitendo cha
kutoka nje wapinzani
wao kisiasa ni
kutojua majukumu yao na kutokomaa
kisiasa hivyo wawo
watawatumikia wananchi wao
bila ya ubaguzi
wowote wa kisiasa.
Hata
hivyo bado kuna
hali ya sintofahamu
ya jinsi gani
mwenyekiti na makamu
mwenyekiti wa halmashauri
hiyo ushindi walioupata
kwasababu kwa mujibu
wa idadi ya
wajumbe walitakiwa kuwa
17 sasa kura
ya 18 ilitoka wapi
na kuna madai
kuwa Afisa Tarafa
wa Kaisho Godian Rugaimukamu ambaye
alikuwa mwenyekiti wa kikao
alipiga kura na
alipotafutwa hakukanusha wala
kukubali.
No comments:
Post a Comment