Waendesha pikipiki maarufu kama bodaboda wameiomba
serikali kutatua changamoto wanazokumbana nazo
pamoja na kuwapunguzia faini wakati dreva anapokuwa na kosa kwani kipato
chao ni kidogo wanachopata kutokana na
kazi hiyo.
Hayo yamesemwa na baadhi ya waendesha
bodaboda Disemba12 mwaka huu ambapo wamesema kuwa miundombinu ya barabara
imekuwa changamoto kubwa kwao kwani kuna sehemu ambazo barabara ni mbaya,
ikiwemo na kupunguziwa faini kulingana
na kosa mtu analokuwa nalo kwani wamekuwa wakitozwa faini ya kiasi cha pesa
ambacho nikikubwa na kipato chao kiko chini sana.
Naye mwenyekiti msaidizi wa
waendesha pikipiki Fashiru Abdul amesema kuwa anaiomba serikali iendelee kutoa
elimu kwa watumiaji wa pikipiki kwani kumekuwa na watu wanaoendesha pikipiki
bila kujua sheria za barabarani na kusababisha ajali kwa sababu ya kutokuwa na elimu juu ya
uendeshaji wa pikipiki pamoja na sheria za barabarani.
Aidha Abdul amewaomba
waendesha pikipiki kuwa makini barabarani na kupunguza mwendo kasi katika kipindi hiki cha sikukukuu
kwani kuna msongamano mkubwa wa watu ili
kuweza kujiepusha na ajali.
No comments:
Post a Comment