Jamii
wilayani Karagwe kwa
kushirikiana na viongozi wa
kisiasa,dini,mashirika ya kiraia
na serikali wametakiwa
kuungana kwa pamoja
kuhakikisha wanafuatilia matumizi
ya pesa za
mpango wa kunusuru
kaya maskini zinazotolewa
kwa walengwa kama
zinatumika ipasavyo na
kutoa matokeo yaliyokusudiwa na
Mfuko wa Maendeleo
ya Jamii yaani TASAF.
Kauli hiyo imetolewa
katika kikao cha
wadau wa maendeleo
kilichofanyika katika ukumbi
wa kituo Rafiki
cha Vijana maarufu
kama Angaza kilichopo
mjini Kayanga ambapo kikao
hicho kilichoitishwa na mfuko
wa Maendeleo TASAF
kwa ajili ya
kujadili changamoto na mafanikio
ya utekelezaji wa
Mpango wa kunusuru
Kaya maskini awamu
ya tatu.
Wamefikia
uamuzi huo wakati wakipitisha
maadhimio ya kikao
hicho ambacho kilibaini kuwepo baadhi
ya walengwa kutumia
ruzuku zao za
msingi kinyume na
makusudi ya mpango
wa kunusuru kaya
Maskini TASAF Awamu
ya tatu wamesema
moja ya changamoto
ni kuzitumia katika
starehe kwa kunywa pombe
bila kufanya shughuli
yoyote ya maendeleo.
Aidha, Mkuu
wa wilaya ya
Karagwe Karagwe Deodatusi
Kinawiro ameagiza wataalamu
wa TASAF wilaya
ya Karagwe kuhakikisha
wanamuondoa mara moja
mke wa diwani
mmoja ambaye ametajwa
kwenye kikao hicho
kuwa ni mmoja
wa walioingizwa kwenye
mpango huo hivyo
kuagiza aondolewe na
kutakiwa kurudisha pesa
yote ambayo ameishapokea
kutoka mpango huo.
Pia ameagiza watendaji
wote wa vijiji,kata na maafisa Tarafa kuhakikisha
wanasimamia kwa karibu
malalamiko yanayotolewa na
akina mama kufanyiwa
manyanyaso kwasababu ya
kupokea pesa hiyo
ya mpango wa TASAF.
Kwa upande
wake Elias Sowani
ambaye ni mshauri
mwelekezi wa TASAF
wilaya ya Karagwe
akieleza sifa na
hatua za kuondoa
mlengwa ambaye anakuwa
amefariki au sababu
nyinginezo za msingi.
Naye mbunge wa
jimbo la Karagwe
Innocent Bashungwa ameshauri
kuangalia upya utaratibu
wa Mpango wa
kunusuru Kaya Maskini
walengwa kupatiwa ujuzi
na miradi ya
kufanya kuliko kuendelea
kuwapatia pesa taslimu
kwasababu siku ikisitishwa watarudia
hali zao za awali.
Hata hivyo washiriki
wa kikao hicho
cha kujadili utekelezaji
wa Mpango wa
kunusuru Kaya Maskini
wameutaka uongozi wa
TASAF na wadau
kushirikiana kwa karibu
kuhakikisha changamoto na
mapungufu yaliyojitokeza kwenye hatua
zilizopita.



No comments:
Post a Comment