Serikali ya wilaya
ya Karagwe imetoa
muda wa mwezi
mmoja kwa wananchi
wilayani Karagwe kujiandaa
kusitisha shughuli za
uvuvi wa samaki
kwenye maziwa yote
yanayopatika ndani ya
wilaya kwani kuanzia
mwezi wa pili
shughuli zote za
uvuvi zitasitishwa kwa
kipindi cha miezi sita.
Agizo hilo limetolewa
leo na mkuu wa wilaya
ya Karagwe Deodatus
Kinawiro katika kikao
cha wadau wa
maendeleo kilichojumuisha viongozi
wa dini,mashirika ya
kiraia,wananchi na wataalamu
mbalimbali wa halmashauri
ya wilaya ya
Karagwe.
Kinawiro
amesema awali walitangaza
shughuli zote zingesitishwa
kuanzia Januari mosi mwaka
huu lakini kuna
malalamiko yalitolewa na
wananchi kuwa imekuwa
ghafla na hawakupewa
muda wa kujiandaa
hivyo wamesikiliza malalamiko
hayo na kutoa
fursa hiyo ya kujiandaa.
Amesema
ratiba ya kusitisha shughuli za
uvuvi kwenye maziwa
yanayopatikana kwenye wilaya
ya Karagwe itakuwa
ya kudumu kila
mwaka kwa kipindi
cha kuanzia januari
hadi mwezi wa
sita
Hata hivyo ametoa
onyo kwa wananchi
kutotumia kipindi hiki
cha kujiandaa kinyume
na taratibu na
sheria zinavyotakiwa vinginevyo
atakayebainika sheria dhidi
yake zitachukua mkondo
wake.

No comments:
Post a Comment