Na Mbeki Mbeki.
Kyerwa
Mkuu
wa Wilaya ya Kyerwa Mkoani Kagera Luteni Kanali (Mstaafu) Benedict Kitenga
amesema Wilaya hiyo inakabiliwa na changamoto mbalimbali ikiwemo Uhamiaji
haramu, uharibifu wa mazingira na mnyauko bacteria wa migomba.
Hayo
yalisemwa jana na Mkuu wa Wilaya hiyo wakati akizungumza na waandishi wa habari ofisini kwake.
Luteri
Kanali (Mstaafu) Kitenga alisema kuwa Wilaya yake inakabiliwa na changamoto
mbalimbali ambazo alizitaja kuwa ni
uhamiaji haramu ambapo alisema kuwa asilimia 40 ya wakazi wa Wilaya hiyo ni
watu kutoka Uganda, Rwanda na Burundi.
Aliongeza
kuwa katika kata ya Kibingo, Murongo, na Kaisho asilimia 70 ya wakazi wa kata
hizo ni wahamiaji haramu kutoka nchi
jirani, aliongeza kuwa changamoto nyingine ni pamoja na uvuvi haramu, uharibifu
wa mazingira ambao umekithiri kwa kiasi
kikubwa.
Alizitaja
changamoto nyingine kuwa ni magendo ya Kahawa kwenda nje ya nchi mnyauko bakteria wa migomba mnyauko fuzari
unaoshambulia Kahawa uwindaji haramu na Ugonjwa wa Ebora.
Pia
kuwa Wilaya hiyo inakabiriwa na
changamoto ya utekaji wa magari ya abiria na migogoro ya ardhi kuwa vitendo hivyo
visipodhibitiwa vinaweza kuharibu uchumi wa Wilaya na Taifa kwa ujumla.
Kitenga
alisema kuwa uhamiaji huo haramu unaweza pia kuathiri mradi
wa NIDA kuhusu utolewaji wa vitambulisho kwa watanzania kutokana na
mwingiliano wa watu kuwa mkubwa hasa kwa
wilaya zilizo mpakani.
Aidha
Mkuu huyo wa Wilaya alisema kutokana na Takwimu za sensa mwaka 2002 Wilaya hiyo
ina wakazi zaidi ya laki nne na kuwa inasadikiwa kwa Sensa ya watu na makazi ya
mwaka 2012, kwa ongezeko la watu kwa asilimia 2.9 idadi yao itakuwa ni zaidi ya
laki sita.
Hata hivyo amewataka wakazi
wa Wilaya hiyo kushirikiana na Serikali kudhibiti vitendo vya uhamiaji
haramu, ambapo alisema kuwa Mkoa wa
Kagera unasadikiwa kuwa na wahamiaji haramu 18,000.
No comments:
Post a Comment