
Gari lililokuwa limepakia abiria baada ya ajali
Askari usalama wa barabarani wakichukua maelezo eneo la tukio.
Ni ajabu lakini huwezi amini ni gari lililokuwa limebeba abiria.
Watu nao wafika kutoa msaada wa uokoaji
Taarifa za awali kulingana na mwandishi wetu Sospiter Rugemalira aliyekuwa katika eneo la tukio muda mfupi baada ya kutokea kwa ajali hiyo na watu waliopoteza maisha papo hapo ni watu 2 na majeruhi 14 wamekimbizwa katika hospitali ya mkoa wa Kagera.Ajali hiyo imetokea mapema asubuhi katika eneo la mwanzo Mugumu nje kidogo ya mji wa Bukoba likihusisha gari aina ya Hiace ambapo namba zake za usajili hajajulikana ambapo hufanya safari zake kati ya Mtukula na Bukoba.Jitihada za kumtafuta kamanda wa mkoa wa Kagera kuthibitisha tukio hili zinaendelea na ikiwa tayari tutawajulisha kinachoendeleaKamanda wa mkoa wa Kagera Philipo Alex Karangi amethibitisha waliopoteza maisha ni watu 2 na majeruhi ni watu 14 tu
No comments:
Post a Comment