KARAGWE
Halmashauri ya wilaya ya Karagwe mkoani Kagera inakabiliwa na changamoto
mbalimbali katika sekta ya Elimu ikiwemo upungufu wa miundo mbinu ya vyumba vya
madarasa na nyumba za walimu.
Hayo yalibainishwa jana na Katibu wa
mfuko wa Elimu Leofanston Lwangoga ambaye pia ni kaimu katibu wa chama cha
Walimu (CWT) wilayani Karagwe wakati alipokuwa akisoma taarifa ya kikosi kazi
cha elimu (Karagwe education task force) kwenye mkutano wa wadau wa elimu
wilayani humu.
Lwangoga akisoma taarifa hiyo alisema
kuwa changamoto zinazoikabili sekta ya elimu wilayani kwake ni pamoja na
upungufu wa miundo mbinu ya vyumba vya madarsa,nyumba za walimu, maktaba,
mabweni, maabara na majengo ya utawala.
Alizitaja changamoto nyingine kuwa ni
pamoja na kutokuwepo kwa samani za kutosha kama meza, madawati na kabati ambapo
aliongeza kuwa Ikama ya walimu kutotosheleza mahitaji , upungufu wa vitaqbu vya
kufundishia na kutotosheka kwa mlo wa mchana kwa wanafunzi walio wengi kwenye
shule za msingi na sekondari.
Alibainisha baadhi ya mapungufu katika
sekta hiyo kuwa ni vyumba vya madarasa 857, kuwa vilivyopo ni 872 na
vinahitajika 1729 katika shule za msingi huku nyumba za walimu zikiwa na
upungufu 1449 zilizopo 309 na zikihitajika 1758.
Katika shule za sekondari alisema kuwa
vinahitajika vyumba 73, vilivyopo ni 60 na kuna upungufu wa vyumba 13, ambapo
aliongeza kuwa nyumba za walimu zinahitajika 300 zilizopo ni 32 na kuna
upungufu wa nyumba 267.
Kwa upande wake Mkurugenzi Mtendaji wa
halmashauri hiyo Bosco Nduguru alikiri kuwepo kwa changamoto hizo na kuongeza
kuwa wananchi walio wengi hawatambui kuwa wao ni wamiliki wa shule hali
inayosababisha washindwe kuchangia elimu na kuwachukua wazazi wenye watoto
shuleni.
Nduguru alisema changamoto nyingine ni
bodi na kamati za shule kutotambua majukumu yake hali inayosababishwa na kamati
hizo kutopewa mafunzo ya mara kwa mara, kuwepo kwa utoro wa rejareja na kudumu
walimu na wanafunzi na watendaji wa kata na vijiji kutowajibika ipasavyo katika
kusimamia masuala ya elimu kwenye maeneo yao.
Alisema changamoto hizo zimetokana na
utafiti uliofanywa na timu ya wajumbe saba toka miongoni mwa wajumbe 16 wa
kikosi kwake cha elimu kilichoteuliwa na Mkuu wa wilaya septemba mwaka jana.
Baadhi ya wadau wa elimu waliohudhuria
katika mkutano huo walisema kuwa kila mdau wa elimu na mwananchi kwa ujumla
analo jukumu la kuchangia Elimu na mwananchi kwa ujumla analo jukumu kuchangia
elimu kifedha ili kuinua kiwango cha elimu wilayani humo ambapo ulibuniwa
utaratibu wa kubaini wachangiaji uhamasishaji jamii, uandaaji na usambazaji wa
vitabu vya makusanyo na uchangishaji.
Walisema kuwa fedha itakayo kusanywa
itagawanywa kurudishwa kwenye kata kulingana na kiwango kitakachokuwa
kimewasilishwa na kata husika kwa kuzingatia asilimia zitakazowekwa ambapo
wakusanyaji wakuuu wa michango hiyo ni maofisa watendaji wa kata wakisaidiana
na watendaji wa vijiji.
Aidha walipendekeza fedha hizo baada ya
kukusanywa zigawanywe kw uwiano asilimia 60 zipelekwe kwenye kata kwa ajili ya
maendeleo ya elimu, asilimia 30 zipelekwe mfuko wa elimu na asilimia 10
ziingizwe kwenye mfuko wa Halmashauri kwa ajili ya dharula kama vile maafa.
Hata hivyo wameitaka Halmashauri hiyo
kufanya mkakati huo kuwa endelevu kuanzia April hadi mwaka huu ambapo walisema
kiasi cha shilingi 2,465,7000,000 kinahitajika katika kukabiliana na changamoto
hizo.
No comments:
Post a Comment