Mhe. Rais Kikwete na Mhe. Rais Obama wakitembea kwa pamoja.

Mke wa Rais Mama Salma Kikwete na mgeni wake Mama Michelle Obama muda
mfupi baada ya kuwasili kwa Rais Obama nchini kwa ziara ya siku mbili
nchini.
Mhe. Rais Obama akiongozana na Mkuu wa Majeshi wa Tanzania, Jenerali
Davis Mwamunyange mara baada ya kukagua gwaride la heshima.
Mhe. Rais Obama akikagua Gwaride la Heshima
Mhe. Rais Obama na Mhe. Rais Kikwete wakisikiliza nyimbo za Mataifa yao zilizopigwa kwa Heshima ya Rais Obama.
Mhe. Ali Mohammed Shein, Rais wa Serikali ya Mapinduzi Zanzibar, Mhe.
Mizengo Pinda, Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mama
Salma Kikwete, Mama Michelle Obama na Viongozi wengine wa Serikali
wakiwa Uwanjani hapo wakati wa mapokezi.
Mhe. Rais Obama akiwa na Mwenyeji wake Rais wa Jamhuri ya Muungano wa
Tanzania, Mhe. Jakaya Mrisho Kikwete pamoja na mkewe Mhe. Mama Salma
Kikwete na Mama Michelle mara baada ya kupokelewa.

Rais Dkt.Jakaya Kikwete akiwa na mgeni wake Rais Barrack Obama wa
Marekani muda mfupi baada ya kuwasili katika uwanja wa ndege wa
Kimataifa wa Mwalimu Julius Nyerere jijini Dar es Salaam jana
mchana.nyuma ya Rais na mgeni wake ni Mke wa Rais Mama Salma Kikwete na
mke wa Rais wa Marekani Mama Michelle Obama.

Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete akimtambulisha kwa Rais Barrack Obama wa
Marekani Rais wa Zanzibar Dr.Ali Mohamed Shein muda mfupi baada ya
kuwasili katika Uwanja wa Ndege wa kimataifa wa Mwalimu Nyerere jijini
Dar es Salaam jana mchana.Huku Mke wa Rais Mama Salma Kikwete na Mke wa
Rais wa Marekani Michelle Obama Wakiangalia

Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete akimtambulisha kwa Rais Barack Obama wa
Marekani Rais wa Zanzibar Dr.Ali Mohamed Shein muda mfupi baada ya
kuwasili katika Uwanja wa Ndege wa kimataifa wa Mwalimu Nyerere jijini
Dar es Salaam leo mchana.Huku Mke wa Rais Mama Salma Kikwete na Mke wa
Rais wa Marekani Michelle Obama Wakiangalia

Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete akimtambulisha kwa Rais Barrack Obama wa
Marekani makamu wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Iddi muda mfupi baada ya
Rais huyo wa Marekani kuwasili nchini kwa Ziara ya kikazi ya siku
mbili.

Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete akimtambulisha kwa Rais Barrack Obama
Spika wa Baraza la Wawakilishi Zanzibar Padu Ameir Kificho katika uwanja
wa ndege wa Mwalimu Julius Nyerere jana mchana.

Rais Barack Obama wa Marekani na mkewe Michelle Obama wakipokewa kwa shangwe Ikulu, jijini Dar es Salaam.
Rais Kikwete akiwa ameambatana na mgeni wake, Rais wa Marekani,
Barack Obama, wakati wakielekea kuzungumza na wanahabari Ikulu, jioni ya
jana.


Raisi Barack Obama wa Marekani na Rais Kikwete wa Tanzania wakijibu
baadhi ya maswali kutoka kwa waandishi wa habari waliohudhuria mkutano
uliofanywa na Rais Obama na Kikwete mara baada ya kuwasili Ikulu Jijini
Dar jana mchana.
(Picha na Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa na Freddy Maro-IKULU)
No comments:
Post a Comment