Wanawake wanachama wa Karagwe Women Saccos
(KAWOSA) Wilayani Karagwe wameshauriwa kufahamu mambo ya kuzingatia wakati wa
kutoa mikopo ikiwa ni pamoja dhana za mkopaji ziwe na uwiano na thamani ya
mikopo.
Kauli hiyo ilitolewa jana mjini Kayanga
Wilayani hapa na Mwezeshaji wa mafunzo wa mada ya Utawala wa mikopo na
Ujasiliamali Mbatta kutoka chuo kikuu cha Ushirika Moshi (MUCCOBS) katika ukumbi wa (CCM), kwa kushirikisha wanachama wa KAWOSA wilayani hapo.
Simeon alisema kuwa wanawake wanachama wa KAWOSA wanapaswa kufahamu mambo mbalimbali ya kuzingatia wakati wa kutoa mikopo, ambapo alitaja mambo hayo kuwa ni pamoja na mikopo kutolewa kwa wanachama hai walio na akiba inayohusu kukopa.
Alitaja mambo mengine ya kuzingatia wakati wa kutoa mikopo kuwa ni maombi yote ya mikopo yaidhinishwe na Kamati ya Mikopo isipokuwa mikopo ya viongozi kuwa lazima ijazwe na kila mwombaji na mwombaji atoe taarifa ya uwezo wa kulipa mkopo anaoomba.
Alitaja mambo mengine ya kuzingatia wakati wa kutoa mikopo kuwa ni maombi yote ya mikopo yaidhinishwe na Kamati ya mikopo isipokuwa mikopo ya viongozi kuwa lazima ijazwe na kila mwombaji na mwombaji atoe taarifa ya uwezo wa kulipa mkopo anaoomba.
Aliongeza kuwa wanachama kwa pamoja ndiyo wanaohusika na kuwepo kwa mikopo mibaya kwani wao kwa pamoja ndiyo wanaoshiriki kwenye kuweka misingi ya chama kwa kupitisha masharti, sera na
miongozo mbalimbali ya uendeshaji wa chama.
Alisema kuwa athari zinazotokana na ucheleweshaji wa mikopo ni kutopata riba kupunguza mtaji wa chama, na chama ilivyopangwa kutokana na kuwepo fedha kidogo na kupunguza kasi ya mzunguko wa mikopo.
"Kwa ujumla ucheleweshaji wa mikopo ni kama ugonwa kwani ni rahisi kuzuia kuliko kutibu, hivyo unatakiwa ushirikiano wa karibu zaidi kati ya Kamati ya mikopo, mkopaji na mdhamini aidha ni vema wanachama wakaelimishwa juu ya uwiano wa mikopo mibaya na iliyopo kwa nia ya kujua mikopo ambayo haitalipwa" alisema Simeon.
Katika hatua nyingine alisema kuwa ulikuepika ucheleweshaji wa mikopo, Kamati ya mikopo inatakiwa kukutana na kujadili kwa pamoja wakati wa kupitisha mikopo ili kuhakikisha kuwa mikopo hiyo imetoka kihalali na kuwa Mtunza fedha ahakikishe kuwa anatoa taarifa ya kila mwezi kwa ajili ya malingainisho kwenye Kamati ya mikopo ili waweze kupendekeza njia za ukusanyaji mikopo
hiyo.
Alisema Kamati ya mikopo haina budi kuangalia kwa undani uwezo, tabia na dhamana ya mkopaji na wadhamini wake ili mkopo uweze kurejeshwa kwa kufuata kanuni ya 88 (1 -5) na kanuni ya 90 (2).
Mmoja wa washirika katika mafunzo hayo Saada ABdallah alisema kuwa sababu zinazomfanya mwanachama kushindwa kurejesha mikopo ni uchukaji wa fedha nyingi zaidi ya mahitaji halisi, kutopatikana mikopo kwa muda mwafaka, uwepo wa sera dhaifu na kutumia mikopo kwa malengo tofauti.
Aidha Rehema Mtawala wakati akichangia mawazo katika mada hiyo alisema kuwa mwanachama mwenye mkopo uliocheleweshwa aarifiwe mara moja kwa maandishi mapema iwezekanavyo ili aweze kutoa sababu za kutolipa deni lake na wadhamini wapewe nakala kwa ajili ya ufuatiliaji.
Hata hivyo mwezeshaji wa mafunzo hayo amewataka wanachama wa Ushirika wa akiba na mikopo savings and credit cooperative society (SACCOS) kuzingatia kanuni ya 92(1) ya kanuni za ushirika za mwaka 2004
kinachoeleza kuwa mikopo ndani ya chama isizidi 3/4 (robo tatu) ya mtaji wa Ushirika.
No comments:
Post a Comment