Thursday, September 19, 2013

ELIMU NDIO NGUZO MUHIMU INAYOHITAJI UWEKEZAJI ZAIDI KUNUSURU TAIFA

Na 
  Juhudi    Felix
Karagwe 
Wazazi wilayani Karagwe wametakiwa kuwekeza katika elimu kwa kuwapeleka watoto wao katika mashule mbalimbali baada ya kuhitimu elimu ya msingi na sekondari vikiwemo vyuo vya ufundi. 

Hayo yalisemwa jana na mwanachama wa KARAGWE WOMEN SACCOS (KAWOSA) ambaye pia ni mwenyekiti wa umoja wa wanawake Tanzania (UWT) wilayani Karagwe Bi Rehema Mtawala wakati alipokuwa akizungumza na wanachama wa chama cha akiba na mikopo katika ofisi cha chama hicho. 

Bi mtawala alisema kuwa wazazi hawana budi kuwekeza katika elimu kwa kuwapeleka watoto wao katika mashule mbalimbali na sekondari vikiwemo vyuo vya ufundi Alisema kuwa wazazi na walezi wanalo jukumu la kujiunga na vyama vya akiba na mikopo ili kupata uwezeshaji wa kuwalipia gharama za shule na walezi “ 

Kuna baadhi ya wazazi na walezi wamekuwa wakitoa visingizio vya kukosa karo ya shule na mahitaji mengine hii ni kutokana na wao kutojiunga na vyama vya mikopo na kuendelea kutegemea kipato chao ambacho hakiwezi kutosheleza “ Alisema Mtawala. 

Alisema pamoja na uzalishaji kutokana kilimo na shughuli ndogondogo za uzalishaji haziwezi kutosheleza mahitaji ya gharama za shule bila kujiunga na vyama vya akiba na mikopo. Kwa mujibu na maelezo ya Bi. Mtawala alisema taifa la Tanzania linahitaji wataaluma katika sekta mbalimbali wakiwemo walimu madaktari katika sekta zote kutokana na kupeleka watoto wao shule. 

Alisema wataaluma hao hawatapatikana kama wazazi hawatalipa umuhimu suala la elimu katika jamii na vizazi vijavyo havitakuwa na msaada kwa taifa lao. 

Aidha alisema siyo lazima vijana wote wanaohitimu elimu ya sekondari kwenda kidato cha tano na kuongeza vilevile waliohitimu darasa la saba kuwa wanafunzi hao wapelekwa katika vyuo vya ufundi kupata utaalamu mwingine 

Hata hivyo amewataka vijana waliohitimu katika mashule mbalimbali kujiepusha na makundi mbalimbali ya uvutaji wa madawa ya kulevya ulevi na ujambazi bali wajihusishe na shughuli za kulijenga taifa

No comments:

Post a Comment