Na
Juhudi Felix
Karagwe
Watanzania wametakiwa kuwekeza
katika elimu kutokana na mabadiliko na maendeleo ya kiuchumi, kisiasa na
kiteknolojia ndiyo yanayofanya ulimwengu kubadilika kwa kasi kubwa
Hayo yalisemwa jana na Kamishina wa
Polisi Saimoni Siro katika hotuba
ya uzinduzi rasmi wa shule ya msingi Kazoba akimwakilisha Waziri wa mambo ya
ndani Daktari Emmanueli Nchimbi aliyekuwa amealikwa kama mgeni rasmi
katika hotuba iliyosomwa Kayanga
wilayani Karagwe mkoani Kagera.
Siro alisema kuwa wananchi hawana
budi kuwekeza katika elimu kutokana na mabadiliko na maendeleo ya kiuchumi,
kisiasa na kitechnolojia ndiyo yanafanya ulimwengu kubadilika kwa kasi
kubwa ambapo aliongeza kuwa kila binadamu anayetaka kuishi na kupata mafanikio
kuendeana na mabadiliko hayo.
Katika hotuba hiyo alisema kama
ambavyo wengi wao wanafahamu hali ya dunia inabadili kila kukicha kuwa dunia
miaka hamsini iliyopita ni tofauti sana na dunia hali kadhalika dunia ya miaka
hamsini ijayo itakuwa tofauti ilivyo sasa.
Alisema elimu ndiyo msingi kwa
kuendana na kazi ya mabadiliko yanayotokea nchini na duniani kote kuwa lazima
kila mmoja wao bila kujali umri, jinsi au hadhi yake awe tayari kujifunza kila
siku.
Alieleza kuwa kwa watoto wao elimu
bora ndiyo urithi wenye maana ambao utawafanya waweze kukabiliana na
changamoto za kimaisha katika dunia ya kisiasa inayoongoza na teknolojia.
Alisema ili kufanikiwa kiuchumi
kijamii na kisiasa ni lazima wawe na elimu bora itakayowawezesha kujiamini
kitaifa na kushirikiana kwa manufaa yao na nchi yao kuwa msingi wa
kujiamini unatokana na elimu bora inayotolewa katika mazingira bora kama ya
shule hiyo.
Siro alisema uwekezaji huo ni
kielelezo cha utashi wa wamiliki wa shule hiyo kujua changamoto
zinazowakabili kitaifa na kimataifa kutokana na ukweli kuwa hali ya elimu yao
bado siyo kuridhisha sana.
Alisema ni lazima wakubali kutoka
katika hali hiyo ya kuwapeleka nje ya nchi na badala watafute suluhisho la
matatizo yao elimu kwa kuwekeza katika miundo mbinu.
Alifafanua kuwa ni vema watu wenye
uwezo kiuchumi wakirie kuwekeza katika sekta nyingine za kiuchumi unapaswa
kuendana na uwekezaji katika elimu kuwa madhara ya kutowekeza katika elimu ni
pamoja na kuwafanya watoto wao nje ya soko la ajira kwa kukusanya uwezo wa
kushindana na uwezo wa mataifa ya nje.
Aliongeza kuwa shule hiyo iendelee kuzingatia na
kuwafundisha maadili mema kwa watoto kujali utu mshikamano na uzalendo
kwa taifa lao kuwa elimu bila maadili haitasaidia sana kama taifa.
Katika hatua nyingine Siro alisema nchi
inayochangamoto kubwa ya usalama hasa katika mikoa ya mipakani hasa kubwa na
uhalifu hasa ujambazi na utekaji wa magari uvamizi wa mapori hivyo uliwataka
wananchi kushirikiana na serikali kudhibiti matendo hayo haramu.
Kwa upande wake mkurugenzi wa shule
hiyo James Peter Kazoba alisema kuwa shule hiyo ni pekee katika mkoa wa kagera
inayofundisha masomo ya kifaransa ilianza mwaka 2008 ikiwa na jumla ya
wanafunzi 7 tu.
Kazoba alisema shule hiyo ni ya
mchipuo wa lugha ya kiingereza darasa la kwanza hadi la saba na gharama ya shilingi
bilioni moja zimetumika katika uwekezaji wa ujenzi wa majengo ya shule hiyo.
Aidha katika uzinduzi wa shule
uliohusisha pia maafari ya darasa la saba wanafunzi wavulana 5 na wasichana 15
wamehitimu darasa la saba mwaka huu kwa mara ya kwanza ambapo shule hiyo ikiwa
ni ya tatu katika ufaulu wa mtihani wa majaribio darasa la saba kati ya shule
212 za wilaya hiyo.
Hata hivyo alizitaja changamoto
mbalimbali zinaikabili shule hiyo binafsi ya kutwa na bweni kuwa ni pamoja na
ukosefu wa bwalo la chakula, jiko na baadhi ya wananchi kuvamia ardhi ya shule.
No comments:
Post a Comment