a Daniel Limbe,Bukoba
SIKU chache baada ya mgodi wa dhahabu wa Tulawaka uliopo wilayani Biharamulo mkoani Kagera kutangaza kufunga shughuli za uzalishaji dhahabu kwa madai ya kuongezeka kwa gharama za uendeshaji,mapya yameanza kuibuka na kudaiwa kuwa mahusiano mabovu na jamii inayozunguka mgodi huo yamechangia hali hiyo.
Nyingine ni watu wenye silaha ndogo zilizozagaa kutoka nchi jirani kuingia ndani ya mgodi na kutishia usalama wa watumishi wakitaka kupora dhahabu kinyume cha sheria.
Hata hivyo Rweyemamu alisema mgodi wa Tulawaka kupitia mpango wake wa uwajibikaji kwenye shughuli za jamii umechangia ujenzi wa shule ya sekondari Nyantakara,maabara ya kisasa kwenye shule ya sekondari Mavota hali iliyoongeza uwezo wa wanafunzi kupenda masomo ya sayansi.
Pia alisema mgodi huoulichangia ujenzi wa vyumba vya madarasa 16, nyumba 8 za walimu, mabweni 2 ya wasichana, kisima cha maji, meza za walimu, Bwalo la chakula, jiko na jengo la utawala.
Vingine ni viti 689 kwa matumizi ya wanafunzi, meza 11 za ofisi za walimu, na zingine 16 za madarasani, kabati za walimu, meza 50 na mabenchi 100 kwa ajili ya bwalo la chakula, vitanda vya Banco na uwanja wa michezo huku akidai kuwa mradi wa ujenzi wa sekondari ya Nkantakara umegharimu shilingi milionii 542,455,000 zilizotolewa na Tulawaka iliyopo chini ya Barrick.
Aidha mgodi wa Tulawaka ulichukua hatua za kupeleka mafunzoni walimu (vijana) 17 waliokuwa wakijitolea kufundisha kwenye shule za Mavota na Mkunkwa, kupata mafunzo kwenye chuo cha Ualimu Nyamahanga wilayani Biharamulo ili kupunguza tatizo la walimu katika wilaya hiyo.

Akizungumza
na waandishi wa habari Meneja mkuu wa mgodi huo,Filibert Rweyemamu,
alisema mbali na kuongezeka kwa gharama za uendeshaji,wananchi wamekuwa
wakihujumu shughuli za mgodi huo huku wengine wakitumia silaha kali
kutishia maisha ya wafanyakazi.
Taarifa zinaeleza kuwa baada ya mgodi wa Tulawaka kulia na hujuma hizo,ambazo walidai zimekuwa zikiwasababishia kupata hasara kubwa,tayari mgodi huo umeshakabidhiwa kwa shirika la Madini nchini (STAMICO) ili kuuendeleza.
Rweyemamu
alisema sababu nyingine zilizosababisha mgodi huo kunyanyua vilago ni
Misuguano na jamii ya watu wanaozunguka mgodi huo kudai hawaoni faida ya
kuwepo kwa wawekezaji hao hali iliyozua migogoro mingi ya ardhi,baadhi
ya wananchi kuvamia maeneo ya mgodi na kuathiri shughuli za uzalishai
mali.Taarifa zinaeleza kuwa baada ya mgodi wa Tulawaka kulia na hujuma hizo,ambazo walidai zimekuwa zikiwasababishia kupata hasara kubwa,tayari mgodi huo umeshakabidhiwa kwa shirika la Madini nchini (STAMICO) ili kuuendeleza.
Nyingine ni watu wenye silaha ndogo zilizozagaa kutoka nchi jirani kuingia ndani ya mgodi na kutishia usalama wa watumishi wakitaka kupora dhahabu kinyume cha sheria.
Hata hivyo Rweyemamu alisema mgodi wa Tulawaka kupitia mpango wake wa uwajibikaji kwenye shughuli za jamii umechangia ujenzi wa shule ya sekondari Nyantakara,maabara ya kisasa kwenye shule ya sekondari Mavota hali iliyoongeza uwezo wa wanafunzi kupenda masomo ya sayansi.
Pia alisema mgodi huoulichangia ujenzi wa vyumba vya madarasa 16, nyumba 8 za walimu, mabweni 2 ya wasichana, kisima cha maji, meza za walimu, Bwalo la chakula, jiko na jengo la utawala.
Vingine ni viti 689 kwa matumizi ya wanafunzi, meza 11 za ofisi za walimu, na zingine 16 za madarasani, kabati za walimu, meza 50 na mabenchi 100 kwa ajili ya bwalo la chakula, vitanda vya Banco na uwanja wa michezo huku akidai kuwa mradi wa ujenzi wa sekondari ya Nkantakara umegharimu shilingi milionii 542,455,000 zilizotolewa na Tulawaka iliyopo chini ya Barrick.
Aidha mgodi wa Tulawaka ulichukua hatua za kupeleka mafunzoni walimu (vijana) 17 waliokuwa wakijitolea kufundisha kwenye shule za Mavota na Mkunkwa, kupata mafunzo kwenye chuo cha Ualimu Nyamahanga wilayani Biharamulo ili kupunguza tatizo la walimu katika wilaya hiyo.
No comments:
Post a Comment