Na
Juhudi Felix
BUGENE –KARAGWE
Wazazi na walezi wametakiwa kutoa fursa sawa kwa watoto wao
kupata elimu kuliko kutoa upendeleo kwa
watoto wa kiume tu kwani elimu ndio
uwekezaji muhimu wa mkobozi wa mtu yeyote bila kujali jinsia yake.
Kauli hiyo imetolewa na Mkuu wa mkoa wa Kagera Kanali
mstaafu Fabiani Massawe ambaye alikuwa mgeni rasmi katika mahafari ya sita ya
kuwaaga wahitimu wa darasa la saba katika shule ya kiingereza ya Mtakatifu
Peter Claveri wakati akihotubia wanafunzi,wazazi na wageni waalika katika
mahafari hayo.
Amesema kuwa elimu ndio ukombozi pekee kwa mtu yeyote,hivyo
na kuwataka wazazi kutokuwa na dhana ya kusema kuwa watoto wa kike hawana
msaada wowote kumbe hali ni tofauti kwani watoto wa kike ndio wanaosaidia
wazazi wao zaidi kuliko watoto wa kiume.
Huku akitolea mifano mbalimbali ya
baadhi ya wanawake waliofanikiwa kushika nafasi za juu za uongozi miongoni mwaoni spika wa Bunge la Jamhuri ya
Muungano w Tanzania Anna Makinda ,Rose Migiro ambaye alikuwa naibu katibu mkuu
wa Umoja wa Mataifa na mkuu wa wilaya ya Karagwe kuwa hawakupewa nafasi hizo
kwa upendeleo bali wamesoma ndio maana wakashika nafasi hizo.
Amewataka pia wahitimu kuwasaidia wazazi katika kipindi
chote watakachokuwa wanasubiria matokeo yao ya mtihani walioufanya wa
kuhitimu elimu yao ya msingi,na kuwataka
kutojihusisha matendo maovu kwani
wamelelewa katika maadili mema ya dini hivyo kuyaendeleza wakati wote wa maisha
yao ili kuyafikia malengo yawliyonayo.
Amewataka pia walimu kuzidisha malezi yao ya awali ili
kuendeleza heshima na hadshi ya kazi hiyo kwani kipindi cha nyuma mwalimu
aliheshimiwa sana katika jamii na walitunzwa bila gharama kutokana na kutimiza wajibu wao tofauti na
hivi sasa ambapo mwalimu amepoteza hadhi yake kutokana na kutotimiza wajibu
wake sawasawa kama ilivyokuwa mwanzo.
Amelishukuru kanisa
na taasisi zake kwa kuendelea kutoa huduma kwa jamii hivyo kuisaidia
serikali katika jitihada za kuhudumia jamii kikamilifu,na kuongeza kuwa katika
mtihani wa kumaliza elimu ya kidato cha nne shule zinazomilikiwa na kanisa
ndizo ziliongoza kwa matokeo mazuri huku akitolea mfano shule ya mtakatifu
Franciss ya mkoani Mbeya iliyoshika nafasi ya kwanza kitaifa.
Aidha,katika mhafari hayo kumefanyika harambee ya kuchangia
ujenzi wa sekondari ya Mtakatifu Peter Cleveri ambayo inatarajiwa kujengwa eneo la Kihanga kuanzia mwaka wa 2014 ambapo
eneo la heka 33.69 tiyari limeishapimwa kwa ajili ya ujenzi.Katika
harambee hiyo kiasi cha pesa Taslimu 598,200 zilipatikana huku ahadi ikiwa ni
sh 5,170,000 jumla ya ahadi na taslimu
ni sh 5,768,200.
Wahitimu wa mwaka huu ni jumla ya wanafunzi wapatao 32 kati yao wanafunzi wa kiume ni 19 na
wanafunzi wa kike ni 15 ambapo ni mahafali ya sita tangu shule hiyo kuanzishwa na kujivunia kuwa na ufaulu mzuri
ndani ya wilaya mkoa hata Taifa kwa ujumla.
Hata hivyo amewataka wananchi kuwekeza zaidi katika elimu
kwani ndio pesheni ya uzeeni iliyobakia
kwa maana wazazi kipindi hicho huwa wameishiwa nguvu za uzalishaji mali
na watoto wao ndio watakao wasaidia kuwatunza.
No comments:
Post a Comment