Sunday, January 3, 2016

CHANDARUA ZATUMIKA KUSOMBEA MAZAO SHAMBANI BADALA YA KUJIKINGA NA MBU.

Mama   mmoja  ambaye  jina  lake  halikutambuliwa  mara  moja  katika  kijiji  cha  Nyabwegira  Kata  ya  Ndama  wilayani  Karagwe  Mkoani  Kagera  amekutwa  na  kamera  ya  Mtandao  huu akiwa  amebadili  matumizi  ya  Chandarua  zinazotolewa  na  serikali  kwa  ajili  ya  kujikinga  na  mbu  waenezao ugonjwa  wa  malaria   badala  yake  anaitumia  kusombea  maharage  kutoka  shambani.

Afisa  Mtendaji  wa  Kata  hiyo  David  Itegereze   alipomhoji  alisema  alikuwa  hajui  kama  ni  kosa  na  kusema  anazi  nyingi  za  ziada.

No comments:

Post a Comment