Wednesday, March 7, 2012
WALIMU WAPYA WILAYANI KARAGWE WAAHIDIWA KULIPWA IJUMAA WIKI HII
NA Shaaban Ngarama
Walimu wapya waliovamia ofisi ya Mkurugenzi wa halmashauri ya wilaya ya Kargwe wakishinikiza kulipwa stahiki zao machi 6 mwaka huu wameahidiwa kulipwa kabla ya mwisho wa wiki hii.
Hayo yamejiri baada ya Mkurugenzi wa halmashauri hiyo Bw Ernest Kahabi kufika Radio Karagwe kujibu matamshi ya mwenyekiti wa chama cha walimu (CWT) wilayani hapa bw Fredrick Kabendwe kuwa wanampa miezi miwili alipe stahiki hizo vinginevyo wataanzisha mgomo.
Takriba walimu 15 walionekana kuingia ofisini kwa Mkurugenzi huyo na kung'ang'ania kukaa humo hadi watakapolipwa hali iliyopelekea Mkurugenzi bw. Ernest Kahabi kukimbia ofisi na kuelekea Murongo kama alivyothibitisha mwenyewe akidai kuwa ni harakati za kutatua tatizo hilo.
Wakizungumza na radio Karagwe, walimu hao walisema kuwa walidanganywa kwa muda mrefu juu ya malipo yao na kudai wamechoshwa na ahadi zisizotekelezwa. Akizungumzia sakata hilo mkurugenzi Kahabi alisema kuwa ni ucheleweshwaji tu wa malipo hayo kwani baada ya kufuatilia alitaarifiwa kuwa fedha zilishaingizwa katika mpango na akawataka walimu hao kusubiri ili fedha hizo wapewe kabla ya Ijuumaa wiki hii.
Walimu hao walibakia ofisini kwa mkurugenzi hadi pale jeshi la polisi wilayani hapa likivalia kiraia lilipoingilia kati suala hilo na kuwashawishi walimu hao kuondoka ambapo walipewa Tsh 25,000/= kila mmoja kama malazi na chakula wakitakiwa kurudi kwenye vituo vya kazi na kusubiri malipo yao.
Je Ijumaa malipo hayo yatakuwa tayari? kama hayatalipwa nini kitatokea? fuatilia habari zaidi..........

No comments:
Post a Comment