Saturday, March 10, 2012
Malipo ya Walimu wapya Karagwe bado kitendawili!
Na Shaaban Ngarama, Na Tumaini Anathory-Karagwe, Kagera.
BAADA ya walimu wapya kuandamana na kuvamia ofisi ya Mkurugenzi mtendaji wa Halmashauri ya wilaya ya Karagwe na kugoma kuondoka ndani ya ofisi hiyo hadi watakapolipwa madai yao, Ahadi ya kulipya kabla ya mwisho wa wiki hii imegonga mwamba. Radio Karagwe Jumatano wiki imemtafuta Naibu waziri wizara ya Elimu na mafunzo ya ufundi Mh. Fillip Mulugo kujua kinachoendela juu ya malipoa hayo ambapo amedai kuwa tayari fedha hizo zilishaingia mkoani. Mh Mulugo alisema kuwa Katibu Tawala wa mkoa wa Kagera (RAS) ametihbitisha kupokea fedha hizo na pia akaeleza kuwa tatizo liko katika Halmashauri ya wilaya ya Karagwe. ''Kwa habari tulizonazo ni kwamba nadhani watakuwa wamepokea karibu milioni 200, hizi district by district (wilaya kwa wilaya) kwa mfano Karagwe zitakuja kiasi gani huko bado sijazipata, lakini kama nilivyokueleza walimu wanaweza kurest assured (Kuhakikishiwa) kwamba baada ya hii taarifa kwa mfano nimemtafuta mimi RAS nimempata na aka-confirm kwamba zimeingia kwa hiyo matumaini yangu ni kwamba kuanzia kesho(yaani alhamisi) au kesho kutwa (yaani Ijumaa) hapo walimu watakuwa wameshapewa hayo malipo yao" alisema Mulugo.
Machi 10 mwaka huu radio Karagwe imewatafuta baadhi ya walimu kutaka kujua malipo hayo kama yamelipwa ambapo imebainika kuwa wote waliofuatilia hakuna aliyelipwa. Mmoja wa walimu hao Bw.Lenatus Malamala wa Nkwenda amesema kuwa hawajapewa chochote zaidi ya shilingi elfu 25 walizopewa siku ya Jumanne Machi 06 katika kuwashawishi kuondoka ofisini kwa Mkurugenzi. Kauli ya Mh. Mulugo ilienda sambamba na kauli ya Mkurugenzi wa halmashauri hii Bw. Ernest Kahabi aliyedai kuwa watalipwa ndani ya wiki hii."Jana (yaani jumatatu) hela imeingia kwenye mtandao. Kwa hiyo tunatarajia wakati wowote kuanzia leo (Jumanne) na kuendelea hadi kufikia Ijumaa (machi 9) nadhani hela zao zitakuwa zimeshalipwa,ndio jitihada,ndio tunavyofanya sasa, tumechangamka zaidi"! alisema Kahabi. Walimu hao wanaendelea kusubiri bila kujua nani amekwamisha hela hiyo kati ya RAS au halmashauri. Huenda fedha hizo mwanzoni mwa wiki hii zitatolewa.

No comments:
Post a Comment