Tuesday, March 20, 2012

NIDHAMU LAZIMA IWE KWA KILA MTU


Bodi za shule  binafsi zahimizwa  kusimamia nidhamu za watumishi

Na Shaaban Ndyamukama

Bodi ya  shule ya sekondari ya  RHEC English Medium iliyoko wilaya ya Ngara mkoani Kagera imetakiwa kujiamini na kusimamia nidhamu ya shule na watumishi kwa  kukaa vikao hatimaye  kutatua  migogoro kati ya utawala na watumishi  ili kuepuka hasara kwa shule wanafunzi na wazazi wao

Hayo yamebainika jana katika mkutano wa wazazi  na uongozi wa bodi ya shule hiyo wakati wa kupokea taarifa ya ajali ya moto ulioteketeza mali zote za wanafunzi katika vyumba viwili vya bweni la wasichana lenye uwezo wa kulaza wanafunzi 80 wiki iliyopita wilayani Ngara.

Mmoja wa wazazi  katika mkutano huo Bw Josiasi Kimuga amesema kuwa  bodi ya shule inayoongozwa na Mwenyekiti wa kamati ya huduma za jamii katika halmashauri ya wilaya ya NgaraThomson Seyongwe  kijisimamia na kutoa maamuzi kuliko  mtu mmoja au kundi la watu wachache na kukwamisha utoaji wa taaluma  katika shule yake  

 Bw Kimuga amesema kuwa kukosekana kwa vikao vya kutatua migogoro na kutoa maamuzi kumesababisha hata kukosekana muhtasari wa mkutano wa wazazi na bodi mwaka jana ambao ulitakiwa kutunzwa na katibu  ambaye ni mkuu wa shule. Alisema kuwa migogoro iliyopo shuleni  isipotatuliwa haraka wazazi watapoteza wanafunzi wao kitaaluma au hata kuwapotezea maisha na wajumbe wa kamati ya shule ya msingi na bodi ya  sekondari wasimamie majukumu yao kwani ndio wanaowakilisha wazazi

Akitoa taarifa ya moto Mkuu wa shule hiyo Bw Venanti Verdiani amesema moto uliounguza bweni la wasichana ilisababisha hasara  kwa mali za wanafunzi na shule kwa  thamani ya shilingi miliono 152.48 
                                                   
 Alisema katika ajali ya moto huo nusu ya bweni lenye vyumba viwili viliteketea na mali za wanafunzi zenye thamani ya shilingi milioni 14.6 , vitanda 72 viliungua vinavyokadiliwa kwa shilingi kwa Tsh milioni 9.79  na bweni lenyewe nusu iliungua na ukarabati wake pekee utagharimu Tsh milioni 45.36
Alisema kuwa juhudi za haraka zilifanyika ambapo wasamalia wema na uongozi wa shule ni waliweza kutoa magodoro na mavazi pamoja na mahitaji mengine ya kila sikukwa wanafunzi waliounguliwa bweni lao na thamani yake ni Tsh. mil 18.4

Alisema kuwa  utafiti wa kujua chanzo cha moto unaendela kufanyika chini ya vyombo vya dola likiwemo jeshi la polisi na wanafunzi wote 15 waliokuwa wamelazwa katika Hospitali ya Rulenge wilayani humo kwa mshituko waliruhusiwa baada ya afya zao kurejea katika hali yao ya kawaida na amewashukuru wakazi wa Rulenge na wauguzi kwa msaada walioutoa kuokoa maisha ya wanafunzi      

Kwa upande wake Meneja wa shule hiyo Helena Adriani ambaye ni Mwenyekiti wa CCM wilayani Ngara alitoa hali halisi ya migogoro ya shule hiyo kuwa ni walimu upande wa wa shule ya msingi kuwa na utovu wa nidhamu hali iliyosababisha hata wengine kupigana shuleni  na kumwaga chakula cha wanafunzi wao
Alisema kuwa walimu hao walikuwa hawafundishi kwa kuanzisha migomo baridi na kuwafanya wanafunzi kukosa zaidi ya mada katika masomo ambapo juhudi za haraka zilifanywa na walimu wa sekondari kufundisha wanafunzi wa shule ya msingi hadi  usiku
Alisema baadaya kuwepo uvunjifu wa amani katika shule yake aliwaodoa kazini walimu saba na watumishi wengine watatu tarehe  03 mwezi huu na siku chache ndipo bweni likaungua na kusababisha hasara kubwana yeye alikuwa safarini mkoani Dodoma
Aidha Meneja huyo alisema changamoto nyingine katika shule hiyo ni ukosefu wa fedha za kutekeleza miradi mbalimbali kama kujenga uzio kupata huduma bora ya maji kwa wanafunzi kwani michango ya shule ndiyo inayosaidia kuleta maendeleo ya shule yake

‘Nawasihi wazazi kulipa karo kwa wakati na katika kufunga muhula wa kwanza Aprili mosi mwaka huu watakaokuwa bado kulipa karo nitawafukuza sitawapokea muhula wa pili mwezi mei  kwani walimu wanahitaji mishahara na gharama za chakula kulisha wanafunzi zimepanda sana’.Alisema Meneja

Hali hiyo ilimfanya Mbunge mtaafu Angas Gwassa Sebabili kuutaka uongozi wa shule kuweka uzio na walinzi wenye sifa watakaolinda mali za shule na maisha ya wanafunzi Sebabili aliwataka  wazazi kulipa fedha za michango mbalimbali na karo kuwaandaa watoto wao kukabiliana na ushindani wa kielimu na uchumi katika shirikisho la Jumuia ya Afrika ya Mashariki vinginevyo watakuwa watazamaji na vibarua kwa watakao toka nchi nyingine wanachama wa shirikisho la jumuia hiyo
Alisema wanaotafuta elimu kwa sasa ni gharama na zile shule za serikali taaluma yake haiko katika mfumo wa kupata ajira bali inawaandaa wananchi wake kuwa watawaliwa kwa kuwapa elimu isiyoweza kuwaingiza kwenye ushindani na utandawazi  uliopo
‘Elimu ndiyo dira ya kumkomboa  mwanajamii yeyote duniani kama mtapuuzia kutoa michango au kulipa karo kwa wanafunzi nyie ndio mtakaojuta na watoto wenu kuishi nao nyumbani wakiwa watu wazima’.Alisema Sebabili
Wazazi wameshauri ujenzi wa bweni utakaofanyika uweke miundombinu ya kukabiliana na majanga na majengo ya bweni yasiwekewe nomdo katika madirisha na milango ya kufungia kwa nje kwani ili kuepukana na hatari ya kupoteza maisha ya wanafunzi
Shule ya RHEC English Medium ina wanafunzi 617 kati ya hao 324 wanasoma sekondari na 293 ni wanafunzi wa shule ya msingi ambapo kwa sasa imejengewa uzio uliofikia hatua ya nusu ya eneo la shule kwa gharama ya Shilingi milioni 7.52      

No comments:

Post a Comment