UJENZI WA CHUO KIKUU WILAYANI KARAGWE ENEO LA KISHOJU
KUTAKUWEPO VITIVO VYA ELIMU, KILIMO, MAZINGIRA NA BIASHARA
NA JUHUD FELIX
Zaidi
ya shilingi milioni 800 zinatakiwa kukamilisha ujenzi wa Chuo Kikuu
cha kanisa la Kilutheri Dayosisi ya Karagwe kinachotarajiwa kuanza
ujenzi wake Juni mwaka huu.
Hayo
yamesemwa jana na mchungaji Daktari Brighton Katabaro ambaye pia ni
mratibu wa uanzishwaji wa chuo kikuu Karagwe wakati akisoma taarifa ya
azma na mchakato wa uanzishwaji chuo kikuu alipokuwa akizungumza na
waandishi wa habari ofisini kwake Kayanga wilayani hapa.
Daktari
Katabaro alisema kuwa ili kukamilisha ujenzi wa chuo kikuu hicho zaidi
ya shilingi milioni 800 zinatakiwa ili kusiwepo na kukwama ujenzi
utakapoanza katika kata ya Kihanga kijiji cha Kishoju wilayani
Karagwe.
Daktari
alisema kuwa fedha hizo zitapatikana kutokana na michango mbalimbali ya
wananchi ,Taasisi za kiserikali ,na zisizo za kiserikali pamoja na
kuchangia kwa njia ya harambee ili kufanikisha azma ya ujenzi wa chuo
kikuu.
Alisema
kuwa Dayosisi inayo ardhi kubwa na ya kutosha kabisa kwa ujenzi wa chuo
kikuu zaidi ya hekta 372 zilizoko katika kijiji cha Kishoju,kuwa
dayosisi ya Karagwe inaazimia kuanzisha chuo hicho chenye mchepuo wa
kilimo na stadi za mazingira ili kuchangia kuinua hali ya maisha ya
watanzania haswa wanaoishi vijijini wakitegemea kilimo na ufugaji kama
uti wa mgongo wa maisha.
Aidha
Daktari Katabaro alisema kuwa chuo kikuu cha Karagwe yaani Karagwe
Universty College(KARUCO) kitasaidia kuchochea matumizi ya zana za
kisasa za uzalishaji na hivyo kuongeaza tija na kuboresha mazao mengi ya
kilimo yanayozalishwa wilayani hapa.
Kwa
upande wake Askofu Daktari Benson Bagonza alisema kuwa chuo hicho
kitatoa fursa nyingi kwa wananchi zinazolenga kutokomeza umaskini
zikiwemo fursa ya elimu,Kiuchumi, kibiashara,kimiundo mbinu,kiafya na
kimawasiliano.
Daktari
Bagonza alisema kuwa licha ya kilimo na ufugaji chuo kikuu
kinakusudia kuandaa walimu wenye shahada na stashahada katika sanaa
,sayansi na biashara ili kuongeza idadi ya walimu hasa katika shule
za sekondari wilayani Karagwe.
Hata
hivyo Daktari Bagonza alisema dayosisi itaendelea na jitihada za
kushirikisha wadau mbalimbali hapa nchini na nje ya nchi ili kupata
fedha za kutosha kwa ajili ya ujenzi wa chuo hicho kuwa wapo wafadhili
wa nje waliokwisha waunga mkono na kuonyesha dalili za kushirikiana na
dayosisi katika mchakato huo.
No comments:
Post a Comment