Saturday, March 10, 2012

KARAGWE ILIYOGEUZWA SHAMBA LA BIBI



MKUU WA MKOA WA KAGERA  KANALI MSTAAFU   FABIAN MASSAWE

TUME  iliyokuwa ikiwachunguza wafanyakazi wa  Halmashauri ya Wilaya ya Karagwe Mkoani
Kagera waliokuwa wakikabiliwa na tuhuma za matumizi mabaya ya madaraka  pamoja na ubadhilifu wa fedha za Sekondari imekamilisha uchunguzi wake likiwemo jeshi la polisi ambapo Serikali imetoa
tamko la kuwajibika.

Akisoma walaka  uliotoka katika ofisi ya Waziri ya Mkuu Tamisemi Mkuu wa Mkoa wa Kagera
Kanal Mstaafu  Fabian Massawe katika kikao cha dharula cha baraza la madiwani wa Halmashauri ya Karagwe jana alisema kuwa mwaka 2010  watumishi wapatao kumiwa Halmashauri hiyo  walikumbwa na kashfaza kutumia madaraka vibaya na ubadhilifu wa fedha za Umma ambapo tume iliunda
kutoka  ofisi ya waziri mkuu Tamisemi ilikuwachunguza watumishi hao ili kubaini ukweli.

Alisema wakati  uchunguzi ukiendelea, uhamuzi ya kuwa watumishi hao wapumzishwe ilikupisha uchunguzi huku ofisi ya kamanda wa polisi mkoani Kagera iliagizwa naSerikali kufanya uchunguzi pia ili watumishi hao watakaobainika kuwa na makosawaweze kufikishwa mahakamani.

Kanali Mstaafu Massawe alisema kuwa baada ya uchunguzi wa tume na polisi kukamilika Serikali imewachukulia hatua zifuatazo ambapo Mhandisi Christian ambaye anadaiwa  kuingizi hasara Serikali kwa kuibia Halmashauri kiasi cha shilingi Milioni 46 za kutengeneza barabara kwa kushirikiana na mkandarasi na kushiriki katikaupotevu wa shilingi M1. moja  zakutengeneza makaravati, Henerico Batinoluho aliyekuwa afisa elimu msingi ambayeanakabiliwa   na kosa la kumdang’anya mwajiri wake kuwa na shahada ya udhamili kumbe hana na Froliana Buberwaaliyekuwa afisa tabibu katika kituo cha afya Mulongo anayekabiliwa na kosa laKumwibia mwajiri chakula cha wagonjwa chenye dhamani ya shilingi laki moja.

Aliwataja wengine kuwa ni Mwalimu Fransisca Ishengomawa shule ya msingi Kitengule anayekabiliwa na kosa lla kumwimbia mwajiri nakumsababishia hasara ya shilingi milioni 3.2 na Metson Bartazal aliyekuwa
mtunza stoo  Nkwenda anayekabiliwa nakosa la kumwimbia mwajiri na kumsababishia  hasara ya shilingi laki nne kwa kutoa chakula pungufu kwa wagonjwa ambapo Serikali imemwagiza kitabu Tawala wa mkoa wa Kagera Nassor nimeambiwakuwafikisha watumishi hao watano mahakamani ili wachukuliwe hatu za kisheria.

Wengine  ambaowameshukuliwa hatua za kinidhamu kuwa ni Kalumuna Nkalage aliyekuwa katibu wa
bodi ya utumishi wa Halmashauri hiyo, Dokta Thomas Rutachunzibwa ambaye alikuwamganga  mkuu wa Halmashauri, Dauda Hassanfundi mkuu wa Halmashauri na Mkude Mwakiluma aliyekuwa akihusika na malipo.

Aliongeza kuwa Consolatha Kamuhabwa ambaye alikuwamkurugenzi wa halamshauri hiyo amevuliwa wadhifa huo na kubaki katika kazi yakeya ya awali ya kitaaluma na kuhamishiwa kituo kingine  cha  kazi katika ofisi ya mkoa wa Arusha ambapo imedaiwa kuwa maechukuliwahatua za kiutawala,

Pia alisema kuwa Serikali imejaza nafasi hizo  ambapo watumishi tisa wameisha pewa barua za
uhamisho kuja kuziba nafasi hizo huku wakitarajia kuletwa  mkurugenzi au kumpandisha daraja aliyekuwa
anakahimu nafasi hiyo Ernest Kahabi.

Mkuu wa Mkoa huyo alisema kuwa usimamizi hafifu wanidhamu katika Halmashauri hiyo  imeshuka
kwani watumishi wengine 12  wanakabiliwana kesi za rushwa ziko mahakamni pia wapo watumishi 30
Halmashauri hiyo wanachunguzwa ili wachukuliwe na ahtua za kinidhamu na kisheria.

Aidha alisema kuwa hari hii ya usimamizi hafifuimekuwa ikisababisha wananshi kukosa imani na Halmshauri yao ambapo ameongeza kwamba  hutokana na usimamizi  hafifu wa viongozi huku kamati za kudumu za
Halmashauri hiyo zikiagizwa kufanya kazi ipasavyo na madiwani kutokubalikupokea taarifa zilizoandaliwa ovyo ovyo.

Hata hivyo alisema kuwa mabadiliko hayo yanalengakuijenga Karagwe mpya ni budi kila mtu kuyaunga mkono hususani watendaji namadiwani wa Halmashuri hiyo.

No comments:

Post a Comment