Friday, April 20, 2012

HII NI BAJETI YA WILAYA YA NGARA -KAGERA


Halmashauri ya Ngara kutumia shilingi bil 27.7 Mwaka 2012/2013

Na Shaaban Ndyamukama Ngara

Baraza la madiwani la Halmashauri ya wilaya ya Ngara mkoani Kagera limepitisha bajeti ya mwaka wa fedha wa 2012/2013 kiasi cha Shilingi Bilioni 27 na milioni 772.8 kwa ajili ya shughuli za maendeleo ya wilaya hiyo

Hayo yalibainika Aprili 14 mwaka huu katika mkutano wa baraza la madiwani uliofanyika katika ukumbi wa halmashauri ya wilaya ya ngara wakati wa kupata taarifa ya bajeti iliyosomwa na Afisa Mipango wa wilaya Bw Martin Kanyambo

Martin Kanyambo alisema kuwa kati ya fedha hizo shilingi bilioni moja na milioni 592.7 ni mapato ya ndani na Shilingi Bilioni 10 na milioni 515.09 ni fedha za ruzuku na fedha kutoka kwa wafadhili

Alisema katika mwaka huo wa fedha 2012/2013 halmashauri inatarajia kutumia shilingi Bilioni 12 na milioni 974.2 kulipa mishahara ya watumishi wa halmashauri hiyo huku serikali kuu ikitarajia kutoa shilingi bilioni 7 na milioni 386 kwa ajili ya maendeleo

Alisema kuwa kwa matumizi ya fedha za ruzuku kuanzia mwezi julai 2011 hadi Desemba 2012serikali iliidhinisha Tsh 25, 104 908 721 na kati ya fedha hizo Tsha bil 9.63 zilikuwa ruzuku ya matumizi mengineyo OC na shilingi bil 2.56 ni mishahara ya watumishi huku vyanzo vya halmashauri vikiwa Tsh bil 1.33 pamoja na ruzuku ya miradi ya maendeleo kiasi cha Shilingi bilioni 11.58

Kwa kipindi hicho hicho halmashauri yetu ilipokea kiasi cha Tsh Bil 7,217,498.9 sawa na 29% ya makisio ya ya mwaka kiwango ambacho akikidhi utekelezaji wa miradi ya wananchi na hata kuwa na wakati muguu wa kusimamia majukumu kwa idara zote za Halmashauriwakiwemo watumishi wake wa kada mbalimbali

Wakichangia katika taarifa ya bajeti hiyo wajumbe wa baraza hilo wamezitaka idara ya mipamgo uchumi na fedha kukusanya mapato ya halimashauri kwa uadilifu na kutumia wakusanyaji wa mapato walio waaminifu ili kuleta maendeleo ya haraka kwa wananchi

Diwani wa kata ya Bukiriro Eriki Nilamachumu amesema kuwa baadhi ya Vyanzo vya mapato kama masoko katika sehemu mbalimbali za vijiji hukusanywa ushuru lakini haioneshi fedha hizo zinaelekea wapi na kusababisha kuwepo mianya ya ubadhiliu kutoka maeneo husika. Nkilamachumu alisema kuwa mapato yakusanywe kutoka vituo vya kuegesha magari katika mji wa Kabanga Rulenge Benako na Ngara mjini pamoja na ushuru wa masoko ya Rwinyana keza Kigarama Mikole Kigoi na maeneo mengine ili kukamilisha malengo ya kukusanya milioni 37,9 ifikapo mwezi juni mwaka huu
.
Alisema kuwa mapato kutoka baadhi ya maeneo yamekuwa yakitozwa ushuru wa bidhaa mbalimbali toka kwa wananchi lakini katika mipango na mikakati halmashauri haijaonesha vyanzo hivyo na kuwepo dalili za ubadhilifu kwa watoza ushuru huo na kukosa kuwasilisha kwa kamati na idara husika.Alitaja masoko yanayotoa mapato ya halmashauri na fedha kuishia kwa watoza ushuru kuwa ni maegesho ya magari katika mji wa Kabanga Rulenge Benako na Ngara mjini na masoko ya Rwinya Keza ,Kigarama ,Mikole, Kigoi ,kihinga ,Nyambazi ,Mkalinzi ,Kumwendo na maeneo mengine.

Kwa upande wake Diwani wa kata ya kasulo Philbert Kiiza alidai kuwa halmashauri iweke mikakati na mipango ya kujenga maegesho mapana na yenye kuvutia kwa ajili ya
Alisema kiwango cha sasa cha ushuru wa shilingi 2000 kwa kila gari hakilingani na thamani ya mizigo iliyoko kwenye magari hayo pia fedha iongezwe hadi shilingi 5000 kwa kila roli la mizigo na kwa magari yanayolala benako kuelekea nchini Rwanda pamojana yale ya kabanga kuelekea nchini Burundi

‘’Napendekeza kuanzisha soko katika maeneo ya mnadani kwa kugawa viwanja kwa wananchi na kujenga vibanda vya Biashara vitakavyolipiwa ushuru wa mapato ya halmashauri pamoja na kuimarisha makusanyo ya minada ya Ng’ombe katika eneo la Benako na Murusagamba’’.Alisema Kiiza

Aidha alishauri kuwa ushuru unaotozwa kwa wenye ng’ombe wakiwemo wanaopatikana kwa kumilikiwa na wahamiaji haramu na kuvamia ardhi kisha kuathiri mazingira watozwe faini kwa kuchangia maendeleo hata kwa kujenga chumba cha darasa na kwamba mkurugenzi awe mstari wa mbele kwenda vijijini kutafuta mapato kabla ya agizo la kuondolewa kwa msako maalum




Hata hivyo Menyekiti wa halmashauri hiyo John Shimilimana ameshauri madiwani kusimamia mapato ya halmashauri yao kwa kuhamasisha wananchi kulipa ushuru na wao kutoa taarifa ni wapi mapato yanapatikana kwa muda na eneo husika ili kuleta ufanisi wa halmashauri yao
Amesema kuwa wananchi wahamasishwe kuchangia maendeleo kwa kukusanya vifaa vya ujenzi wa miradi mbalimbali kwenye maeneo yao lakini pia watendaji wawape taarifa nanchi taarifa ya mapato na matumizi kuimarisha utawala bora.Amesema kuwa katika mwaka wa fedha wa mwaka 2010/2011 halmashauri iliidhinishiwa kupata shilingi Tsh 21 ,255,532,987/= na kati ya fedha hizo zilitolewa Ruzuku ya mishahara kiasi cha Tsh 7,687, 376 ,000/=.
Alisema kuwa Ruzuku ya matumizi mengineyo OC ilikuwa niTsh bil 2,milioni 564.28 na mapokezi ya fedha hizo hadi juni 30, 2011 kilikuwa kiasi cha Tsh 14, 821, 965, 900/= sawa na asilimia 70 ya makisio ya mwaka.
Hata hivyo Menyekiti wa halmashauri hiyo John Shimilimana alisisitiza madiwani kusimamia mapato ya halmashauri yao kwa kuhamasisha wananchi kulipa ushuru na wao kutoa taarifa ni wapi mapato yanapatikana kwa muda na eneo husika ili kuleta ufanisi wa halmashauri yao
Aliema kuwa wananchi wahamasishwe kuchangia maendeleo kwa kukusanya vifaa vya ujenzi wa miradi mbalimbali kwenye maeneo yao lakini pia watendaji wawape taarifa nanchi taarifa ya mapato na matumizi kuimarisha utawala bora.Amesema kuwa katika mwaka wa fedha wa mwaka 2010/2011 halmashauri iliidhinishiwa kupata shilingi Tsh 21 ,255,532,987/= na kati ya fedha hizo zilitolewa Ruzuku ya mishahara kiasi cha Tsh 7,687, 376 ,000/=.
Alisema kuwa Ruzuku ya matumizi mengineyo OC ilikuwa niTsh bil 2,milioni 564.28 na mapokezi ya fedha hizo hadi juni 30, 2011 kilikuwa kiasi cha Tsh 14, 821, 965, 900/= sawa na asilimia 70 ya makisio ya mwaka.
Alizitaja changamoto zinazoikabili halmashauri ya wilaya katika kuleta maendeleo ya wananchi wake kuwa ni kucheleweshwa kwa fedha za ruzuku toka serikali kuu na kusababisha utekelezaji wa miradi kuwa chini ya malengo ambapo kwa mwaka 2010/2011 utekelezaji wa miradi ya maendeleo ulikuwa wastani wa 39%
Alidai kuwa kwa matumizi ya fedha hizo halmashauri ilitumia bil 4.29 sawa na 41%ya makisio ya bajeti hali inayowapa wakati mugumu wa watendaji na madiwani kukamilisha miradi ya wananchi mijini na vijijini kwenye halmashauri hiyo

‘Ndugu zangu uchumi wa taifa kwa sasa ni mrama hivyo kila mmoja awajibike kwa kutimiza majukumu yake kwa nafasi aliyonayo kuhamasisha jamii kuchangia na fedha zitakapofika tuzisimamie ipasavyo kwa kuepuka miradi kukwama ama kuchelewa .Alisema Shimilimana
Halmashauri ya wilaya ya Ngara inajumuisha kata 20 na tarafa nne ambazo ni Nyamiaga Rulenge, Kanazi na Murusagamba pamoja na kujumuisha vijiji 72 ikiwa ni moja ya wilaya zinazoathirika na wahamiaji haramu wa nchi jirani Rwanda na Burundi.Ends


No comments:

Post a Comment