Friday, April 20, 2012

UNYANYASAJI KARAGWE WAPIGWA VITA



Jamii wilayani karagwe na mkoa wa kagera kwa ujumla  imetakiwa kuachana na mila na destuli potofu ambazo  zinachochea unyanyasaji kwa  wanawake.

Akizungumza na waandishi wa habari ofisini kwake  Afisa ustawi wa jamii bw LAZARO MAJETA  amesema kuwa kuna baadhi ya  jamii hapa wilayani karagwe ambazo bado zinakumbatia  dhana na mila potofu kwakudai kuwa wanawake hawana sauti yeyote  ya kudai haki zao au kutoa  maoni ambayo yanaweza kuchangia katika suala zima la kimaendeleo .

Hata hivyo bw MAJETA ameeleza kuwa wanawake wamekuwa wakinyanyasika sana katika jamii  kwani hawapewi vipau mbele kama ilivyo kwa wanaume akivitaja   kuwa ni ukosefu wa elimu pia ushirikishwaji katika masula mbalimbali    hususani katika kumiliki ardhi na mashamba hata mali  pindi wanapokuwa wameondokewa na waume zao.

Aidha bw MAJETA hakusita kuzungumzia suala la mahari katika jamii na kusema kuwa suala hilo limepelekea  wanawake  wengi  kunyanyasika katika jamii na hata katika familia zao kwa ujumla kwani wanapotolewa mahari waume zao wanawatumia kama wapendanyo kwa  kudai kuwa amemnunua  kwa  hiyo atamnyanyasa awezavyo  .


Sanjari na hayo bw MAJETA  amewataka wanajamii wote kujua na kutambua  kuwa haki za mwanamke ni haki za binadamu na hivyo basi jamii  haina budi kuwathamini  na kuongeza kuwa  iadara yake imejipanga kuwa chukulia hatua watu wote ambao wanawanyanyasa wanawake.


Baadhi ya wnafunzi wilayani karagwe mjini kayanga  wametaja changamoto mbalimbali wanazokumbanaa nazo  wanapopata mamba wakiwa shule

No comments:

Post a Comment