WANANCHI WILAYANI NGARA WAJENGEWA ZAHANATI NA HDT
KAGERA
Shirika
ka HDT lenye makao makuu jijini Dar es Salaam
limetoa msaada wa jengo la
zahanati katika kijiji cha Mumuhamba
wilaya ya Ngara mkoani Kagera lenye thamani ya TShilingi milioni 50.5
Akikabidhi jengo hilo April 17
kwa uongozi wa Halmashauri ya wilaya ya Ngara kwa niaba ya mkurugenzi wa
HDT DR Peter Bujari Afisa miradi wa shirika hilo la Human
Development
Trust (HDT) mkoaniKagera mchungaji Feres Sendegeya alisema HDT
imejenga zahanati katika kijiji hicho kwa kushirikiana na shirika
rafiki la heath of
Australi and Tanzania (HAT)
Mchungaji sendegeya alisema kuwa mradi wenyewe kwa kujenga
zahanati umegharimu shilingi milioni 49,na laki moja kati ya hiz shilingi ilioni 35.5 sawana
asilimia 81 zimetumika kujenga
Alidai kuwa katika
,usimamizi na ukaguzi ni kiasi cha shilling milioni nne sawa na asilimia tisa
na utoaji wa mafunzo kwa kamati za afya ya kijiji na wahudumuwa afya ya msingi
jumla shilingi milionio 3.7 sawa na 7% na hadi kukabidhi mradi umekamilika kwa
kiasi cha shilingi Mil 50.5 hamsini
Alisema kuwa HAT ndiye mfadhili na
HDT ilisimamia ujenzi kwa lengo
la kusaidia wananchi kuboresha huduma za kijamii na hadi jengo hilo
linakamilika wananchi kwa kutumia nguvu zao hasa kukusanya vifaa
vinavyopatikana kwenye mazingira yao
thamani yake ni kati ya shilingi milioni mbili na laki tano
Aidha aliongeza kwa
kusema kuwa zahanati hiyo itahudumia
wananchi wapatao 5,076 wa kijiji cha Mumuhamba na kati ya hao wanawake ni sawa
na 54% ambao ni kipaumbele cha taifa katika malengo ya millennia
‘Tunaaminikwa hatua hii itasaidia malengo ya millennia
katika utekelezaji wa program ya MMAM na shirika litaendelea na miradi ya afya
katika kijiji hiki maana uwepo wa
zahanati hii shirika litawasiliana na Halmashauri ya wilaya kuondoa changamoto
mbalimbali’.Alisema Mchungaji Sendegeya
Akitoa shukrani kwa niaba ya serikali ya wilaya ya Ngara na
wananchi wa kata ya Bukiriro kilipo kijiji cha Mumuhamba Mwenyekiti wa
Halmashari ya wilaya ya Ngara John Shimilimana
aliwasihi wananchi kuilinda miradi
inayoletwa na wafadhili pamoja na serikali kwani mara inapokamilika inakuwa ni mali yao
Alisema kuwa ili wananchi wapate huduma za afya kila kaya
ijiunge na bima ya mfuko wa afya ili fedha zao ziweze kutumika kununua dawa kwa
haraka huku serikali ikisaidia kuongeza kiwango cha michango yao kwa asilimia hamsini .Alisema
mara baada ya miundombinu itakapokamilika kama nyumba ya kuishi waganga na
wauguzi choo cha wagonjwa na wafanyakazi wengineo halmashauri itakuwa tayari kuwaleta watumishi
toka idara ya afya kwa ajili ya kuwahudumia wananchi.
Alisema kuwa endapo wananchi wataendelea kujitolea kwa
kukusanya zaidi vifaa vya ujenzi
halmashauri itaharakisha kutoa nguvu zaidi kuwaunga mkono katika kuhakikisha
changamoto zilizoko zinaondoka katika kijiji hicho na maeneo ya jirani na
kuwapunguzia mwendo mrefu akina mama wajawazito na watoto chini ya miaka mitano
kutafuta huduma mbali na maeneo yao
Kwa upande wake
Diwani wa kata ya Bukiriro Emily
Nkilamachumu alisema halmashauri ya wilaya isichelewe kuleta wataalamu wa afya
kuhudumia wananchi kwa kuwa vifaa viko tayari na fedha za kusogeza hadi eneo la
ujenzi zimeshatolewa na wananchi wa kijiji hicho. Alidai kuwa wananchi licha ya
kuchangia na kufikia hatua ya jengo kukamilika changamoto iliyopo ni kupata
watumishi wa afya waadilifu wenye kujali maslahi ya wananchi hivyo halmashauri
kupitia ofisi ya Mganga mkuu wa wilaya iwatume wafanyakazi wa afya walio na
moyo wa kujituma katika kutoa Huduma na wenye kuzingatia kanuni za utumishi.
Wananchi wa kijiji cha Mumuhamba kabla
ya kujengewa zahanati hiyo walikuwa wakilazimika kutembea umbali wa kilomita tano hadi kumi
kutafuta Huduma za Afya katika kituo cha Afya cha kata ya Bukiriro na wengine
walikosa dawa kwa kuwa na changamoto za kukosekana katika rejesta ya watumiaji wa kituo hichokinachohudumia
kata nne za tarafa ya Rulenge Ngara
Mkurugenzi wa Shirika la HDT Dr Peter Bujari ambaye ni mzaliwa wa wilay
ya Ngara alianzisha shirika hilo kwa
lengo la kutoa Huduma za kijamii na mpaka sasa limepanuka na kuhudumia baadhi
ya jamii katiak mikoa ya mbeya Ruvuma na kagera hasa kusaidia watoto na
wanawake walio katika mazingira hatarishi
Watoto hao na wanawake hupata msaada wa mitaji ya kuinua maisha yao ikiwa ni pamoja na
kusomesha watoto wa shule za msingi na sekondari walio katika mazingira magumu
kwa kupewa vifaa vya kujifunzia huku walezi wao wakipewa mbinu za ujasiliamali
kupunguza umaskini katika familia .
Katika mkoa wa kagera shirika hilo linatoa Huduma katika wilaya
za Bukoba muleba karagwe Ngara na Biharamulo ikiwa ni pamoja na kusaidia
waathirika wa VVU kwa kuwapa dawa za kuzuia magonjwa nyemelezi na mbinu za
kuwaongezea matumaini ya kuishi na kujumuika na jamii katika shughuli
mbalimbali.
Kwa sasa wigo wa Huduma kwa shirika hilo umepanuka na
kujumuisha kata nane wilayani Ngara ambazo ni Bukiriro, Rulenge ,Rusumo
,Kabanga, Bugarama, Nyakisasa, Muganza na Murusagamba ambapo baadhi ya familia
hupewa mifugo na kuitunza kusomesha watoto na familia nyingine hupewa fedha
taslimu kila kaya shilingi laki moja ili kuwa wajasiliamali.
No comments:
Post a Comment