Watiwa mbaroni kwa udokozi katika
duka wilayani Ngara
Vijana wawili wakazi wa mji mdogo wa Rulenge wilaya ya Ngara mkoani Kagera wamenusurika kuuwawa na
wananchi wenye hasira kali baada ya kudokoa bidhaa kwenye duka la mjasiliamali
katika mji huo jumatatu wiki hii
Vijana hao ni Shabani
Jacobo ( 37) na Godfrey Turbo (27 ) waliingia katika duka la mfanyabiashara
Ismail Mulengera wa mji wa Rulenge kutafuta bidhaa kuwaletea wateja
wake na walipofika ndani ya stoo walianza kukwepesha baadhi ya mali na katika
kuficha ndipo wakabambwa na mwenye duka
Wananchi waliowakamata
waliwakuta na katoni mbili za sabuni na makasha mawili ya amila aina ya
pasha na kuanza kupata kipondo kabla ya madhara kutokea kwao waliokolewa na
polisi jamii kituo cha Rulenge kwa kufungwa kamba katika kuokoa maisha yao na kufikishwa kituo cha polisi
Akiongea na mwanahabari aliyefika eneo la tukio mmiliki wa
duka walikodokoa vijana hao ismail mulengera amesema kuwa amekuwa akiwaamini
kwa kushusha bidhaa katika magari atokapo kahama lakini kila akifanya
majumuisho ya mauzo amekuwa akipata hasara ya mali aliyonunua
‘’Si mimi pekee katika mji huu kuwatumia hawa wabeba kago bali wamekuwa wakitumiwa na
hata wenzangu pia ni ndugu zetu lakini
kwa tabia hii hakuna kuwalea watatutia hasara’’. Alisema Mulengera
Naye mwenyekiti wa mji huo
Saidi Kiveve alisema kuwa vijana hao ni hohe hahe na hivyo mwenye duka
apunguze jazba na kuwasamehe kwani thamani ya mali waliyokutwa nayo ni ndogo
‘’Hawa ni vijana wa hapa na kama ismaili ni Mwislamu
anapaswa kuwasamehe na sisi viongozi wa kijiji kuwaonya si kuwafungakama hasira
zinavyomtuma’’.Alisema mwenyekiti Saidi
Mkuu wa kituo cha polisi cha rulenge ambaye hakutaka jina
lake litajwe gazetini amethibitisha kuwapokea vijana hao na kwamba uchunguzi
dhidi ya tuhuma zinazowakabili utafanyika.Ends
No comments:
Post a Comment