Sunday, February 3, 2013

AGIZO LA UTEKELEZAJI WA MRADI WA UMWAGILIAJI BUJURUGA LATOLEWA

Na Juhudi   Felix
karagwe


Mkuu wa Mkoa wa Kagera Kanali mstaafu Fabian Massawe ameiagiza kampuni ya ujenzi CMG CONSTRUCTION CO.LTD inayoendelea na ujenzi wa mradi wa umwagiliaji Bujuruga ulioko katika kata ya Bugene Wilayani Karagwe  kuhakikisha inakamilisha mradi huo Kabla ya mwezi Aprili la sivyo mkandarasi atalipa fidia kwa Serikali

Alitoa agizo hilo juzi wakati alipofanya ukaguzi wa mradi na kupewa taarifa na mkandarasi wa Halmashauri ya Wilaya hiyo Baraka Sanga kuwa mradi huo ulitegemewa kumalizika Februari mwaka huu lakini mpaka hivi sasa ni asilimi 30 tu ya mradi ndio imekamilika.

“ Sawa yameishatokea inavyoonekana hamataweza kumaliza  kwa muda uliopangwa kwahiyo naagiza katika miezi miwili ijayo asilimia 70 ya mradi iliyobaki iwe imekamilika kama sio sisi tutaanza  kukata faida  ambapo mtakuwa mkitulipa asilimi 18 kila mwezi kwenye milioni 580 mnazopaswa kulipwa,mwezi wa nne mwishoni mnatakiwa muwe mmekabidhi ,tumewaongezea muda pengine mlikwama kutokana na mambo madogo madogo kama vile mvua lakini pamoja na hayo angalia vifaa mnavyotumia vimezeeka mnatakiwa kuongeza  nguvu kakodishe vifaa vinavyoweza kufanya kazi hata kwa wachina mmekuja kufanya kazi hapa”alisema kanali Masawe kwa ukali.

Alisema lengo la Serikali ni kuhakikisha wakulima wananufaika kupitia kilimo cha umwagiliaji kwa kulima kilimo chenye tija na sio cha kuchumia tumbo kwa hiyo Halmashauri ya Wilya ya Karagwe ilitenga milioni 580 ili kuanzisha ujenzi wa mradi wa umwagiliaji  ambao unatarajiwa kuhudumia zaidi ya kaya 300 za kata ya Bugene zinazotegemea kuanzisha kilimo cha mpunga na mazao mengine.

Wakati huo huo katiika taarifa ya mradi iliyosomwa na katibu w amradi huo Fard Hamad kwa niaba ya kamati mbele ya mkuu wa mkoa Massawe alibainisha kuwa wananchi  walioko katika eneo la mradi huo wanaidai kampuni hiyo kiasi cha shilingi milioni kumi kutokana na huduma mbalimbali walizozitoa kwa wafanyakazi wa kampuni hiyo zikiwemo chakula na nyumba za kupanga.

Wananchi hao katika Taarifa hiyo wamemuomba mkuu wa mkoa kuagiza mkandarasi huyo aweze kuwalipa deni la hilo lililodumu kwa zaidi ya miezi minane ili waweze kurudisha mtaji wao na kuendeleza biashara zao.

Kwa upande wa mkandarasi wa Halamashauri ya Karagwe Baraka Sanga alisema kuwa mkandarasi aliyepewa  kazi hiyo hana wasimamizi wazuri “unaweza kuona mkandarasi anayepaswa kuwepo hapa hayupo anawaachia washauri hawajui kazi hii vizuri ,yeye anaacha washauri  ambao  hawana uzoefu na kazi hii mfano aliwaachia watu hawa anaodai kuwa ni makandarasi wajenga wia wakajenga tofauti na mchoro tulipokagua tukawataka wabomoe na kujenga upya kwa kufuata mchoro kwahiyo hari hiyo inatupa taabu pia imechangia mradi kuto kamilika kwa kati”aliongeza Sanga

Kwa upande wa Mhandisi  Marco Mkenda wa kampuni hiyo inayolalamikiwa kutokamilisha mradi kwa wakati na kuwatapeli wananchi kiasi cha shilingi milioni 10 alisema kuwa baada ya mkubwa wake aliyepo Dar es Salaam kupata malalamiko hayo aliamua kumtuma yeye ili aje kutatua tatizo hilo ili mradi uweze kukamalika mapema kama ilivyo pangwa.

“Baada ya bosi makao makuu Dar kupata malalamiko hayoa alinituma nije nione kuna nini ndipo iligundulika kuwa mwenzetu aliyetangulia alipewa pesa ya ujenzi akaitumia visivyo na hata hiyo inayodaiaw ana vibarua pamoja na watoa huduma ila sio kiasi cha milioni 10”alisema Mkenda


Massawe ameagiza kamati ya mradi kukaa na mkandarasi huyo ili kutathimini madeni hayo kisha Halmashauri hiyo ifanye utaratibu wa kuwalipa wadai hao kutoka katika pesa ya mkandarasi huyo pindi atakapo maliza kazi ili kuondoa kero hiyo inayopelekea kuwagawa wananchi na wakandarasi wanaokuja kufanya kazi katika maeneo yao kwa kukosa imani nao.
Amemtaka afisa kilimo wa Wilaya na timu yake kuwaelimisha wakulima juu ya kilimo cha umwagiliaji kupitia mashamba darasa kwani katika Wilaya hiyo ni mara ya kwanza kujihusisha na kilimo cha  huku akiwataka wananchi kuwa karibu na wakandarasi ili waone mradi unavyoendelea ili waweze kuhoji pale penye mapungufu kupitia kamati ya miradi

No comments:

Post a Comment