Thursday, June 27, 2013

MNYAUKO KERO KWA WAKULIMA KARAGWE

     Karagwe
 
Zaid ya Migomba 463,000 imengolewa katika wilaya ya Karagwe na Kyerwa kutokana na ugonjwa wa myauko bakteria unaoshambulia migomba katika kipindi cha mwaka 2006/2013.
 
Kauli hiyo imetolewa jana  na kaimu Afsa kilimo wa wilaya ya karagwe Dominic Eustad wakati alipokuwa akizungumza na waandishi wa habari ofisini kwake
 
Eustadi alisema kuwa migomba 463.000 imeishangolewa katika kata 40 za  wilayani hiyo kutokana na kuathirika kwa ugonjwa mnyauko bakteria unaoathiri migomba ambapo alisema kuwa migomba iliyoathirika ni  764,492 na kaya zilizoathirika ni 31,963 kati ya kaya 108,301 za Wilaya hiyo.
 
Alisema kuwa ugonjwa huo uliingia kwa mara ya kwanza mkoani kagera katika wilya ya Muleba kata ya Izigo mwaka 2006,na kuwa katika wilya ya karagwe mnyauko huo ,uliingia katika kata za Murongo,na Kibingo Wilayani Kyerwa kutokea nchini Uganda.
 
Alisema ugonjwa huo  unaenezwa kutokana na vifaa vya mashambani,wadudu,Ndege ,Wanyama  na kuwa kila kaya inalazimika kutumia vifaa vyake  na kuongeza kuwa Ugonjwa huo hauna dawa ya kutibu au kuzuia kuenea.
 
Alisema kuwa katika udhibiti wa ugonjwa huo,Ofsi yakeinakabiliwa na changamoto mbalimbali ikiwa ni pamoja na mashamba makubwa kukanda na kuchangia katika uenezi wa  mashamba yenye kesi na yaliyotelekezwa  na baadhi ya mashamba ya wazee.
 
Alisema mkulima ambaye  atakayekiuka sharti lililoainishwa katika kifungu cha 7(1)c) cha sheria ndogo atakuwa ametenda kosa na atawajibika kulipa faini kwa Afsa mwidhini au Afsa ugani shilingi 10,000 kwa kila mgomba ambao atashindwa kuukata na kuuzika ili asiambukize ambayo bado haijaambukizwa.
 
Aidha alisema kuwa dalili za ugonjwa huo ni pamoja na majani ya mgomba kubabuka,tunda la mgomba kuiva kabla ya wakati ,ua dume kunyauka na kwenye shina kutoa utomvu ulioganda.
 
Hata hivyo amesema wanasiasa wameanza kuelewa zoezi hilo na kuhamasika kwa kuwaunga mkono maafisa ugani katika udhibiti wa ugonjwa huo ambapo aliongeza kuwa wilaya hiyo inakabiliwa na upungufu wa maafsa ugani.

No comments:

Post a Comment