Na Juhudi
Felix-KARAGWE
Paroko wa parokia ya Kabanga jimbo katoriki la
Kigoma padre John Babitisit Mapunda
ameishauri Taasisi ya kuzia na
kupambana na rushwa TAKUKURU
kuwachukulia hatua wanaokiuka maadili ya
uchaguzi katika kipindi hiki cha kuelekea uchaguzi mkuu.
Ushauri huo ameutoa wakati akizungumza na Radio
Fadeco kwa njia ya simu,Agost 17 mwaka huu,na kusema kuwa TAKUKURU haina budi
kutumia sheria kuwabana wanaotumia fedha kupata madaraka kwani rushwa katika
uchaguzi inaathiri mfumo wa utoaji haki katika Nyanja za za siasa, uchumi na
mazingira.
Mapunda amesema kuwa Rushwa kwa wakristo ni dhambi
ambapo inasababisha kudidimiza uchumi wa Nchi na wanao husika katika kutoa na
kupokea rushwa lazima wathibitiwe.
Amedai kuwa Rushwa kwa sasa inaoneka kuwa ugonjwa wa
ambao hauponi ,badala ya kupungua inaongezeka kupitia Viongozi ambao wange kuwa
watendaji wakuu katika kukomesha vitendo
hivyo.
Amewataka waumini wa madhehebu mbalimbali hapa
nchini wasiburuzwe na wanasiasa bali waijue siasa kwa kutumia akili waliyopewa
na Mungu kwani hakuna dini inayokubali
watu wake wawe maskini katika suala la maendeleo na kuwataka wabadilike kwa kuzisoma harama za Nyakati.
Aidha amesisitiza watanzani kutambua madhara
yatokanayo na Rushwa katika unyanyasaji kimaendeleo kwa kutumia sanduku la kura
kuleta mabadiliko katika nchi kwa kuwa
na utawala bora.
Hata hivyo Mapunda ameongeza kuwa Tume ya Taifa
ya Uchaguzi NEC ihakikishe inaweka nguvu zote kurekebisha kasoro za
vitambulisho vya wapiga kura ili
itendeke haki kwa wote katika kupiga kura muda utakapo wadia.
Hakika ni maadili lazima yazingatiwe
ReplyDelete