Sunday, December 27, 2015

KIJANA MMOJA APOTEZA MAISHA KWA KUPIGWA NONDO KICHWANI AKITOKA MATEMBEZINI YA KRISMANS


Kijana mmoja Wa Mtaa wa Muleba Mjini Wilayani Muleba aliyejulikana kwa jina la Muta Mtalemwa Aliyekadiriwa kuwa na umri wa miaka kati ya 22 na 23, Ameuawa Kwa kupigwa na Nondo Kichwani usiku wa kuamukia leo.




Kifo hicho kimempata wakati alipokuwa akitoka kwa Baba yake Mkubwa akielekea kwa Baba yake ndipo watu wasijulikana walipomvamia na kumpiga na nondo kichwani.


Akizungumuza na KARAGWE FORUM  Mwenyekiti wa Mtaa huo  Panckrasi Mtwara amesema kuwa Mara baada ya kijana huyo kuvamiwa alikimbizwa Hospitalini kwa ajili ya kupatiwa Matibabu na kuwa baada ya muda wa  saa  moja hali yake ilibadilika kufikia alfajili ya leo kijana huyo alikata roho..
  


Aidha, Mtwara ameongeza kuwa Mpaka hivi sasa waliohusika na tukio hilo bado hawajafahamika ingawa vyombo vya ulinzi na usalama vinaendelea na Uchunguzi ili kuwabaini waliohusika huku akiwataka wananchi kuwa wapole katika kipindi hiki kigumu..

No comments:

Post a Comment