Timu ya YANGA imeendeleza ubabe wake katika ligi kuu ya Vodacom kwa msimu wa 2015/2016 baada ya kuifunga timbu ya Mbeya City goli 3-o
Mabao ya YANGA yamefungwa na Amis Tambwe amefunga Mawili na Thabiti Kamsoko amefunga moja.
Kwa matokeo hayo yanga Inafikisha pointi 33 akimwacha mpinzani wake wa Karibu AZAM FC ambayo ina pointi 29 na inacheza kesho na Kagera Sugar kwenye uwanja wake wa nyumbani Chamanzi.
Matokeo mengine Ndanda FC imekubali kipigo cha mabao 3-1 katika uwanja wake wa nyumbani kutoka kwa Jkt Ruvu magoli ya washindi yamefungwa na Saad Kipanga dak 64, na mawili yamefungwa na H.Thabit akafunga dakika 24 na 37 huku la kufutia machozi likifungwa na Atupele Green dakika 46

No comments:
Post a Comment