Sunday, December 27, 2015

POMBE ZA KIENYEJI ZA POTEZA MAISHA YA MTU MMOJA HUKU MWINGINE AKINUSURIKA KIFO.





Wakati  wakristo  na  wananchi  wote  kwa  ujumla  wakiendelea  na  shamrashamra  za  kusherekea  kumbukumbu  ya  kuzaliwa  Yesu  Kristo  ijulikanayo  kama  NOEL  au  Krismansi  mtu  mmoja  mkazi  wa  kijiji  Cha Nyakayanja  kata  ya  Nyaishozi  amekutwa   bafuni  amefariki  dunia.

Aliyekutwa  amefariki  ametambuliwa  kwa  jina  la  Joseph  Kaneganega ambaye  alikuwa  akifanya  kazi  za  ulinzi  kijijini  hapo amekutwa  bafuni wanapofanya  kazi  hali  iliyopelekea  taarifa  kutolewa  kwa  uongozi  wa  kijiji.


Taarifa  za  awali  zimebainisha  kuwa marehemu  Joseph  Kaneganega  amekutwa  na  mabaki  ya  pombe  ya  kienyeji  na  gongo  ya    kienyeji  kwenye  chupa  za  plastiki.

Wakati  huo huo  mkazi  mwingine  atumia  pombe  na  kuzidiwa  hali  iliyopelekea  kukurogewa  kilogramu  mbili  za  sukari  na  kuzinywa  hali  iliyomfanya  azinduke.
 
Afisa mtendaji wa kata Nyaishozi,Nickolausi Burukadi   Kachencha wakati akiongea na wananchi wa maeneo hayo   Desemba 25 mwaka huu,amewaomba wananchi wa Nyakayanja na Mtakuja  kupunguza unywaji wa pombea aina ya Viroba   eti wakidai kuwa wanasherekea sikukuu ya Noel.

Mtendaji huyo amezungumza hayo kutokana na mtu mmoja aliyefahamika kwa jina la Kalingo Amosi mkazi wa kitongoji Mtakuja kijiji Nyakayanja baada ya kunywa pombe nyingi kuzidi kiasi .


No comments:

Post a Comment