Friday, March 2, 2012
AJIRA SI SERIKALIN INAWEZEKANA KUJIAJIRI
Ajira si mpaka serikalini au kwenye taasisi kumbe kuna fursa nyingine za kujiajiri ili kuweza kujipatia kipato cha kukidhi mahitaji yako.Hapa ni Bwana Elias Zakaria 25 ambaye ni mwanakikundi cha BUDAP ambacho kinafanyia shughuli zake KIROYERA TOURS ambayo ni kampuni ya utalii inayojihusisha na utunzaji wa utamaduni wa mkoa wa Kagera.
BUDAP ni kikundi cha walemavu ambacho kilianzishwa mwaka 2005 kinajihusisha na kazi za mikono kama vile utengenezaji wa vifaa vya muziki asilia kama vile ngoma za asili,malimba,na ufundi wa kushona nguo kwa kutumia cherehani.Bwana Elias anabainisha kuwa walianza wakiwa wanakikundi zaidi ya kumi lakini kwa sasa wamebakia wanakikundi sita ,mmoja ni wa kike na watano ni wanaume
Alisema kuwa moja ya sababu zilizochangia kupunguza wanakikundi kuwa baadhi yao walipopata ujuzi waliamua kwenda kuanzisha vikundi ama kufanya shughuli zao binafsi.Akibainisha mafanikio wanayopata ni kuwa wanapata kipato cha kukidhi mahitaji yao kwa kuuza vifaa hivyo kwa wageni wanaofika kutembelea makumbusho hayo
Hii inaonesha kuwa tusiwe tunawanyanyapaa walemavu kwa mtazamo wa baadhi ya watu katika jamii kuwa na dhana potofu ya kuwaona watu wenye ulemavu hawawezi kufanya kazi yoyote kumbe inawezekana wakipewa ushirikiano wa kutosha na kuondoa unyanyapaaji.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment