Sunday, March 17, 2013

LAZIMA KUHESHIMU KANUNI NA TARATIBU ZA MAHALI HUSIKA



 NA
     JUHUDI   FELIX

KAYANGA -KARAGWE

Askari jeshi mstaafu ,raia wa nchi ya uganda Luten Bashiru Karimunda miaka 40,amehukumiwa kwenda jera miaka 2 katika wilaya karagwe kwa kosa la kuingia nchini bila kibali.


Mbele ya hakimu wa mahakama hiyo Peter Matete mwendesha mashitaka  wa polisi  Juma Lipwata ameeleza mahakamani hapo kuwa mshitakiwa aliingia nchini Tanzania tarehe isiyojulikana Oktoba 2012 akitokea nchini Uganda ,na alifikia katika kijiji cha Rwabigaga kata Mabira wilaya mpya ya Kyerwa bila kuwa na kibali.

Awali mshitakiwa nchini Uganda alikuwa askari mstaafu wa jeshi la nchi hiyo mwenye Namba RO 5788 na mnamo mwaka 2012 alipewa cheo cha Luteni katika jeshi la UPDF,mshitakiwa ni mkiga na wazazi wake wote ni raia wa nchi hiyo.

Imedaiwa mahakamani hapo kuwa mshitakiwa mnamo Februaly 27 mwaka huu akiwa Kyerwa aliwekwa chini ya ulinzi na kupelekwa ofsi ya uamiaji Murongo,na mnamo MOSI March  mwaka huu mshitakiwa alipelekwa katika ofsi ya uhamiaji Karagwe,na badaye machi  4 mwaka huu mshitakiwa alifikishwa mahakamani.


Kwa upande wake mshitakiwa alijitetea na kuomba mahakama imsamehe  kwani alifika nchini humo kuhudhuria kesi ya Ardhi yake ambayo ilidhurumiwa na pia ameongeza kuwa kwa sasa ni mgonjwa ambapo anatembelea magongo baada ya kupata maumivu katika mguu wake wa kulia.

Hata hivyo mshitakiwa amehukumiwa kwenda jera  miaka  miwili  baada ya hakimu wa mahakama hiyo kuridhika na ushahidi uliotolewa na upande wa mashitaka .

Akitoa hukumu hiyo Matete amesema kuwa ametoa adhabu hiyo kali ili iwe fundisho kwa wahamiaji wote wasio kuwa na vibari vya kuingia na kutoka nchini.

No comments:

Post a Comment