RISALA YA UZINDUZI WA MIAKA HAMSINI (50) YA UHURU WILAYANI KARAGWE TAREHE 04/11/2011 /20
1.UTANGULIZI.
Mh.Mgeni Rasmi,
Ninachukua
nafasi hii kutoa shukrani zangu za dhati kwako kwa kukubali wito
wakuungana nasi katika sherehe hii ya uzinduzi wa Miaka Hamsini (50)ya
Uhuru Wilayani Karagwe sambamba na Sikukuuu ya Wakulima Nane Nane Mwaka
2011.
1.1 HALI YA WILAYA KWA UFUPI
Wilaya
ya Karagwe ni kati ya Wilaya 8 za Mkoa wa Kagera .inapatikana katika
Latitude nyuzi 1º hadi 20º Kusini ya Ikweta na Longitude 30º hadi 38º.
30” Mashariki mwaGreenwich . Wilaya inapakana na Nchi ya Uganda upande wa Kaskazini, Nchi ya Rwandaupande wa Magharibi, Wilaya ya Ngara upande
wa Kusini na Wilaya ya Misenyi na Mleba upande wa Mashariki. Mto wa
Kagera upo mpakani mwa Wilaya ya Karagwe na Nchi ya Rwanda na sehemu ya
Kaskazini Magharibi mwa Nchi ya Uganda .
Wilaya
ina eneo la Kilimita za Mraba 7,716,kati ya hizo Kilomita za Mraba
7,558 ni eneo la nchi kavu na Kilomita za Mraba 158 ni eneo la maji.
Mwinuko wa Ardhi kutoka usawa wa Bahari ni Mita 1500 hadi Mita 1800.
mwinuko mrefu ni Mlima wa Rwabunuka .Hali ya hewa kwa ujumla ni joto la
wastani wa 20- 26ºC. Mvua zinanyesha kwa wastani wa Milimita 1,040 hadi
1,200 kwa Mwaka kati ya Mwezi September na Januari na kati ya Mwezi
Machi na Mei.
1.2 UTAWALA
Kiutawala
Wilaya imegawanyika katika Tarafa 9, Kata 40 Vijiji 166 na Vitongoji
1,373. Katika mgawanyiko huu, Tarafa 5 Kata 12 Vijiji 57 na Vitongoji
211 ni vipya. Tangu Mwezi Julai 2010 Serikali iliridhia ombi la
kuanzisha Wilaya mpya ya Kyerwa, iliyo na Tarafa 4 Kata 18, Vijiji 93 na
jumla ya Vitongoji 646. Tunayo majimbo 2 ya uchaguzi ya Karagwe na
Kyerwa yaliyo na Wabunge wafuatao:-
- Jimbo la Karagwe- Mhe.Gosbert Blandes (CCM)
- Jimbo la Kyerwa- Mhe. Eustace.O.Katagira(CCM)
1.3 IDADI YA WATU
Kwa mjibu wa Sensa ya Mwaka 2002 Wilaya ilikuwa na watu 423,423.
(Me 207,850 na Ke 215,573). Ongezeko la watu kwa Mwaka ni Asilimia 2.9. Hivyo inakadiliwa kwa kutumia ongezeko hilo Mwaka 2011 Wilaya ilikuwa na idadi ya watu wapatao 639,651.
2. HISTORIA YA WILAYA
Wilaya ya Karagwe ilizinduliwa Mwaka 1958 na Gavana Richard Turnbull baada ya kumegwa kutoka katika Wilaya ya Bukoba.
Kwa hali hiyo Wilaya ya Karagwe ilikuwepo wakati Tanganyika inapata
Uhuru wake hapo tarehe 9/12/1961. Wakati huo shughuli za kiutawala
zilikuwa zinafanyika katika maeneo mawili tofauti yahani Kayanga na
Nyakahanga (yaani Ahalukiko). Baadae Kayanga ikawa ndiyo Makao Makuu ya
kiutawala ambako Mkuu wa Wilaya alikuwa akifanya kazi wakati huo
Nyakahanga palikuwa panatumiwa na Omkama kama Makao Makuu yake.
Kabla
ya Uhuru kulikuwa na utawala wa Ma-chifu (Omukama) na Mabaraza
yaliyojulikana kama Gombolola. Chifu (Omukama ) alisaidiwa na Katikiro
ambaye alikuwa msaidizi wake Mkuu. Chini ya uongozi wa Katikiro
walikuwepo wasaidizi waliojulikana kama Abakungu. Kazi ya Abakungu
ilikuwa ni kuhakikisha amani na usalama vinakuwepo kusimamia na kuhimiza
maendeleo na kutoza kodi ya kichwa.
MUUNDO WA WILAYA WAKATI WA UHURU NA JINSI ULIVYOBADILIKA
Wakati wilaya inaanza waka 1958 ikuwa imegawanyika katika maeneo ya utawala yaliyokuwa yanajulikana kama “subchiefs”. Haya maeneo yalikuwa 7 nayo ni
Bugene – palijulikana kama migongo
Nyaishozi – palijulikana kama kiyanja
Nyabiyonza – palijulikana kama chikuba
Kituntu – palijulikana kama bugabwe
Mabira – palijulikana kama marungu
Kaisho – palijulikana kama buganga (karagwe keifo)
Murongo- palijulikana kama buganga
Kila
“subchief” ilikuwa na kiongozi wake aliyefahamika kama mwami wa
gombolola ambaye alifanya kazi chini ya chifu (omukama wa karagwe).
Mwaka
1965, “subchiefs” hizo ambazo baadae zilikuja kuitwa kata zilizoongezwa
na kuwa 28 hadi mwaka 2010 nazo ni bugene ihanda nyakahanga kiruruma
bweranyange kibondonyakakika kayanga
ndama rugu nyakasimbi ihembe nyaishozi nyabiyonza kihanga kituntu
igurwa mabira kimuri kamuri rwabwere nkenda kaisho isingiro murongo
kyerwa kibingo na bugomora.
Watu
wenye uhalifu mdogo na wenye kesi za migogoro ya ardhi walikuwa
wanahukumiwa kwenye “subchiefs” hizo. Wenye kuhusika na mauaji na kesi
za mogogoro ya ardhi walipelekwa bukoba ambapo omukama alihukumu
kesi/mashauri yaliyowashinda abakungu.
Na pia ziliundwa tarafa 4 ambazo ni
Bugene/nyaishozi
Nyabiyonza
Kutuntu/mabira
Kaisho/murongo
Baada
ya baraza kuvunjwa na machifu kuondolewa,wilaya ilipata mkuu
wa wilaya wa kwanza mwananchi aliyeitwa ndugu Peter
Kafanabo mwaka 1961.Pia alikuwa katibu wa kwanza wa TANU Karagwe.
Halmashauri ya wilaya ya Karagwe
ilaundwa mwaka 1965 wakati huo ikiwa inajulikana kama Buhaya
district council hadi mwaka 1872 chni ya uenyekiti wa ndugu Ferdinand
Mujungu. Baada ya hapo ilivunjwa na kuwa “district development council”
hadi mwaka 1984. mwaka 1984 ndipo ilipoundwa Halmashauri hii ilipo
sasa. Tangu wakati huo wenyeviti wake wamekuwa kama
ifuatayo:-
1.ndugu H.N Kyakatuka 1984-1988.
2.ndugu Salvatory Kalabamu 1989-2005.
3.ndugu S.R kashunju 2006-mpaka sasa.
Pia wakurugenzi wa Halmashauri ya wilaya ya Karagwe tangu ianzishewe mwaka 1984 ni kama ifuatavyo:-
1.Ndugu G.E. KAgaruki 1984-1986
2.Ndugu E.J. Muganda 1986-1989
3.Ndugu T.K. Ndibarema 1989-1992
4.Ndugu O.K. Mwasha 1992-1998
5.Ndugu S.A Masindike 1998-2002
6.Ndugu M.S. Mboje 2002-2006
7.Bibi C.M. Kamuhabwa 2006-2010
8.Bwana E Kahabi (Kaimu) 2010 hadi sasa
HALI YA UONGOZI TANGU 1961
Wilaya ya Karagwe imewahi kuwa na uongozi wa wakuu wa wilaya kama ifuatavyo:-
1.Marehemu PETER N. KAFANABO 1961-1965
2.Marehemu ENOS RYANGARO 1965-1969
3.Ndugu LOSA LIYEMBA 1969-1973
4.Ndugu THOMAS MSONGE 1973-1977
5.Ndugu RUHASI 1977-1978
6.Lt. F.X.ITALA 1978-1980
7.Ndugu RAPHAEL CHAYEKA 1980-1984
8.Marehemu MOHAMED CHAMSALA 1984-1989
9.Ndugu LUHOZYA E.SIWALE 1984-1989
10.Capt. JOSEPH E. NDITI 1989-1997
11.Ndugu GERARD J.GHACHOCHA 1997-1999
12.Ndugu PETER KANGWA 1999-2000
13.Ndugu SANGO OLETELELE 2000-2004
14.Ndugu DAVID J. DAUD 2004-2006
15.Ndugu FRANK UHAHULA 2006-2009
16.Col.Mst FABIAN I.MASSAWE 2009hadi sasa
MATUKIO NA MABADILIKO MAKUU KISIASA, KIUCHUMI, KIUTAWALA, KIULINZI, KITEKNOLOJIA NA KIJAMII.
a) KISIASA
Wilaya ya karagwe ilianzishwa mwaka 1958 chini ya utawala wa wakoloni. Mabadiliko ya kwanza kisiasa yalikuwa ni yale ya
utawala kutoka kwa wakoloni kwenda kwa wananchi wenyewe kupitia uhuru
wetu wa mwaka 1961. aidha viguvugu la mfumo wa vyama vingi vya siasa
lilianza mapema katika harakati za kutaka kujitawala kutoka kwa wakoloni
wa kiingereza na utawala wa kifalme wa kiarabu vyama hivyo ni TANU TAA
AFROSHIRAZ PARTY. Baada ya uhuru uongozi wan chi ulikuwa chini ya chama
kimoja cha TANU na baadaye CCM. Mabadiliko ya sasa ni utawala wa vyama
vyingi vya siasa vilivyosajiliwa ni CCM,CHADEMA,CUF,TLP,na NCCR Mageuzi.
Mwenyekiti wa kwanza wa TANU alikuwa Bwana Kahungya. Waliofuatia tangu
wakati huo ni kama ifuatavyo:-
1. Ndugu Eliakim Kahungya
2. Ndugu Martin Pancras
3. Ndugu Fredinand Majungu
4. Ndugu Hezekiel Kyakatuka
5. Ndugu Gregory Rwabutomize
6. Capt.Salvatory Rwechungura
7. Ndugu Audax Kagaruki
8. Ndugu Justinian Kazungura 2007 hadi sasa.
Aidha Wilaya ya Karagwe iliwahi kuwa na Wabunge wafuatao:-
JINA MWAKA JIMBO
1. Mheshimiwa Gervase Kaneno 1965 – 1968 Karagwe
2. Mheshimiwa Laurent Nyamalaba 1968 – 1975 Karagwe
3. Mheshimiwa Venant Rwabuti 1975 – 1980 Karagwe
4. Mheshimiwa Elikano Byeitima 1980 – 1995 Karagwe
5. Mheshimiwa Sir George Kahama 1995 – 2005 Karagwe
6. Mheshimiwa Eustace O.Katagira 1995 – 2000 Kyerwa
7. Mheshimiwa Mtungirehi 2000 – 2005 Kyerwa
8. Mheshimiwa Gosbert Blandes 2005 – hadi sasa Karagwe
9. Mheshimiwa Eustace O.Katagira 2005 – hadi sasa Kyerwa
b) KIULINZI
Kabla
ya kupata uhuru mwaka 1961, ulinzi wilayani karagwe ulikuwa ni ule wa
jadi.baadae mgambo, askari polisi na vyombo vingine vya ulinzi na
usalama viliongezwa. Mwaka 1978/1979 sehemu ya wilaya ya karagwe ilikuwa
miongoni mwa maeneo yaliyovamiwa na majeshi ya Uganda sehemu ya mpakani mwa Tanzania na Uganda . Kati ya mwka 1993 na 1994, wilaya ilikumbwa na wimbi la wahamiaji haramu kutoka nchi ya Rwanda ambao
walikuwa wanakimbia mauwaji ya kimbari. Wahamiaji haramu haao walifuata
njia zilizopitiwa na Ndugu zao mwaka 1957 – 1962 ambao pia walikuwa
wanakimbia vita vya kikabila.
Athari za matukio haya:-
a) vita vya kagera iliathiri hali ya maendeleo hasa katika sehemu za mpakani katika kata za mrongo, Bugomora na kibingo.
b) Wimbi
la wahamiaji haramu lilipelekea kuongezeka kwa vitendo vya uhalifu na
uharibifu wa mazingira. Mifugo (ng’ombe) waliibiwa kutoka wilayani
kwenda nchi jirani za Uganda na Rwanda kwa wingi maeneo mengi ya karagwe
yalianza kukaliwa na wahamiaji haramu. Nafasi za masomo nyingi hasa
shule za msingi zilijazwa wahamiaji haramu, hata nafasi za kazi za
maofisini na katika sekta ya afya nazo zilijazwa na wahamiaji haramu.
Hata baada ya nchi za Uganda na Rwanda kuwa na amani na usalama wimbi
kubwa la wafanyakazi waliosomeshwa na taifa hili walihamia katika
mataifa yao na kuacha pengo la kiutumishi Tanzania
c) KIUTAWALA
Mwaka
2011 mabadiliko makubwa yaliyotokea na serikali kuridhia mgawanyiko wa
wilaya kutoka kuwa moja hadi kuwa mbili yaani wilaya ya karagwe na
wilaya ya kyerwa. Aidha mabadiliko yafuatayo yametokea baada ya
mgawanyiko wa wilaya ya karagwe.
Tarafa zimeongezeka toka 4 za awali hadi 9 za sasa
-kata zimeongezwa kutoka 28 hadi 40
-vijiji vimeongozwa toka 109 hadi 166
- mamlaka ya mji mdogo wa kayanga imeanzishawa
-waheshimiwa madiwani wa kata mpya walichaguliwa kata uchaguzi mkuu wa mwaka 2011.
d) KIUCHUMI
Mabadiliko
makubwa yaliyotokea kuichumi ni pamoja na kupanuka kwa kilimo ambacho
ndiyo shughuli kuu ya kiuchumi ya wananchi wa karagwe. Uzalishaji wa
kilimo kwa mazao kama ndizi, mahindi, maharage viazi matunda kahawa n.k.
umeongezeka kulingana na kipindi nchi yetu inapata uhuru mwaka 1961.
aidha kabla ya uhuru madini ya TIN yalikuwa yanachimbwa huko kyerwa.
Uchimbaji huo kwa sasa umebakia kwa wachimbaji wadogowadogo tu. Wakati
huo umeme wa kutumia nguvu za maji (HEP)ulizalishwa kutoka kwenye
maporomoko mya mto kagera eneo la mrongo hadi kyerwa “syndicate” kwa
ajili ya kuchimba kusafisha na kubagua TIN. Mitambo hiyo ya umeme
iliharibiwa na Idd Amin wakati wa vita vya kagera 1978 – 1979 .
Hali
ya maaendeleo kiuchumi imekuwa kubwa kwa upande wa kilimo kwani
uzalishaji wa mazao ya chakula na biashara hasa kahawa umeongezeka.
Kukua huku wa uchumi kumeenda sambamba na kuongezeka kwa watu hususani
wahamiaji kutoka wilaya zingine za bukoba muleba biharamulo na ngara.
a) KITEKNOLOJIA
Wakati
Tanganyika inapata uhuru mwaka 1961 hali ya maendeleo ya kiteknolojia
wilayani karagwe ilikuwa duni. Kwa sasa hali imekuwa tofauti kuna umeme,
kuna mawasiliano ya simu za mezani na mkononi, kuna matumizi ya
computer na internet n.k. umeme uliokuwepo kabla ya uhuru ulitoka kikagati Uganda na
kwenda kyerwa kwa ajili ya uchimbaji wa madini ya bati (TIN). Umeme huo
uliondolewa baada ya machimbo hayo kufungwa na matokeo ya vita vya
kagera.
b) KIJAMII
Wakati Tanganyika inapata uhuru, wilaya ilikuwa na huduma chache za kijamii zilizokuwa zikiwafikia watu wachache. Kwa mfano:-
· Kulikuwa
na shule chache sana za msingi lakini pia kulikuwa na shule zilizokuwa
zikijulikana kama middle schools nazo ni lukajange nyaishozi bugene
rwambaizi shule ya kwanza ya sekondari kuanzishwa wilayani karagwe
ilikuwa karagwe sekondari iliyoanzishwa mwaka 1977 na kanisa la
kilutheri na ilianzia katika majengo ya rukajange middle school.
· Kulikuwa na zahanati tatu nyakahanga isingiro na nyakaiga ambazo zote zilikuwa zikimilikiwa na madhehebu ya dini.
· Mawasiliano ya simu hayakuwepo hususani simu za viganja
· Umeme
ulioenea sehemu kubwa ya wilaya haukuwepo umeme wa sasa uliletwa baada
ya vita ya Tanzania na Uganda na hasa katika kipindi cha utawala wa rais
Mseveni
· Huduma ya maji safi na salama iliwafikia watu wachache walioishi mjini kayanga na omurushaka.
1. MAFANIKIO YALIYOPATIKANA TANGU UHURU HADI SASA
a) Elimu
Shule
zimeongezeka sana na hadi sasa wilaya ina shule za msingi 212 na
sekondari 48. kuna vyuo viwili vya ualimu ambavyo vinaendelea kujengwa
na pia kuna mpango wa kujenga chuo kikuu cha kilimo chini ya kanisa la kiinjili la kilutheri .
b) afya
wilaya
ina zahanati 50,kati ya hizo 38 ni za serikali na zilizobaki ni za
binafsi. Vituo vya afya vipo 5,vinne vya serikali na kimoja cha shirika
la dini
c) mtandao
wa barabara za wilaya umeimalishwa na kwa sasa una jumla ya km.
518.7,tabaka la lami nyepesi ni km 13 (kutoka mugakorongo hadi
nyakahanga Hospital) barabara za tabaka la udongo ni km. 384. barabara
kutoka kyaka hadi bugene yenye urefu wa km.59 inajengwa kwa kiwango cha
lami hivi sasa.
d) kuna huduma za uhakika za mawasiliano ya simu
e) kuna huduma ya umeme katika baadhi ya maeneo ya wilaya
f) kuna radio za jamii za FADECO na radio karagwe ambazo zimesaidia jamii kupata habari elimu na burudani.
g) Upatikanaji
wa mafuta aina zote na vyombo vya usafiri na usafirishaji wa uhakika
ambao umewezesha uchumi wa wilaya kukua kwa kasi.
h) Uzalishaji wa mazao ya kilimo na biashara umeongezeka ukilinganisha na watu wa uhuru.
2.
3. CHANGAMOTO
Wilaya ya karagwe bado inakabiliwa na changamoto nyingi ambazo zimekuwa kikwazo kwa hatua kubwa zaidi za maendeleo kufikiwa
Changamoto hizi ni pamoja na :-
a) Wananchi
kutokuwa tayari kuchangia miradi ya maendeleo kwa hiari hivyo
kukwamisha utekelezaji wa miradi mbalimbali ya maendeleo wilayani .
b) Huduma
za jamii hazijaweza kuwafikia wananchi kwa kiasi kinachostahili
mathalani huduma ya maji afya elimu na kadhalika hivyo jitihada zaidi
zinahitajika kurekebisha hali hii.
c) Mamba
za utotoni bado ni tatizo na ni changamoto kubwa inayoikabili wilaya
hivyo juhudi zaidi zinafanyika kurekebisha hali hii, kama vile
kuwapeleka watuhumiwa katika vyombo vya sheria na kuelimisha jamii.
d) Uharibifu
wa mazingira bado pia ni tatizo hasa uchomaji wa moto misitu hatua
mbalimbali zinaendelea kuchukuliwa kurekebisha hali hii hasa kutoa onyo
na elimu kwa wananchi kupitia radio za jamii zilizopo karagwe na
kuchukua hatua za kisheria kwa wanaobainika kutenda vitendo vya
uharibifu wa mazingira.
e) Magendo
ya kahawa kwenda nchi jirani nayo ni changamoto kwa wilaya. Hatua
mbalimbali zimechukuliwa kutatua tatizo hili kubwa zaidi ikiwa ni kuweka
ulinzi wa doria kwa kushirikisha uongozi na jamii katika mialo
iliyobainila kuwa ndiyo vivuko haramu kuvusha kahawa.
4. MATARAJIO
Matarajio
ya wilaya ya karagwe katika kipindi cha miaka 50 ijayo ni kuhakikisha
kuwa huduma za jamii kama vile afya elimu maji n.k. inawafikia wananchi
wote wa wilaya hii.
- kuendelea kuimalisha mawasiliano ya simu ili mitandao ya simu za mikononi iweze kiwafikia wananchi wa vijiji vyote.
- Kuhakikisha kuwa umeme unawafikia wananchi wengi zaidi
- Kutekeleza mipango ya kilimo ili wananchi wa wilaya hii walime kilimo chenye tija na ufugaji bora wa mifugo ya aina mbalimbali.
- Kuinua kipato cha wilaya na cha mwananchi mmoja mmoja hasa kupitia kilimo cha mazao ya biashara, chakula na mbogamboga.
- Kuboresha
kilimo cha kahawa kama zao la biashara kwa kuwapa bei nzuri wakulima
kuimalisha vyama vya ushirika sambamba na uanzishaji wa SACCOS za
wakulima wa kahawa huduma za ugani kudhibiti magendo ya kahawa na
kuhamasisha ununuzi binafsi ili kuleta ushindani wa bei.
- Kuhamasisha
wakulima wapande migomba ya kisasa inayostahimili magonjwa ili kuongeza
uzalishaji wa ndizi kama zao la biashara na chakula.
Naomba kuwasilisha.
No comments:
Post a Comment