NA
JUHUDI FELIX
KARAGWE
Serikali kuu pamoja na halmashauri ya wilaya ya
karagwe , imeombwa kujali masilahi ya walimu, na kushirikiana na Wadau wa elimu
na wazazi ili kupata suluu ya kushuka
kwa kiwango cha ufaulu kwa wanafaunzi wanaohitimu mitihani ya kitaifa.
Hii ni
mingoni mwa maazimio yaliyotokana na mdahalo ulioendeshwa kwa ushirikiano wa mashirika yasiyo ya
kiserikali ya forum syd, karadea, kademvo na MPI{Mwanza
policy initative} na wa dau wa elimu
wilayani karagwe na kyerwa katika ukumbi wa kituo cha habari na mawasiliano
mjini kayanga wilayani karagwe.
Awali wajumbe katika mdaharo huu wamebadilishana
mawazo juu ya nini sababu zilizochangia ufaulu hafifu wa wanafunzi huku
wakibainisha sababu mbali mbali zikiwemo: serikali kutojali maslahi ya waalimu,
ukosefu wa nidhamu kwa wanafunzi, serikali kuingiza siasa katika elimu,
kutowasilikisha waalim katika kutayarisha mitaala na sera za elimu, wazazi au
jamii kwa ujumla kutowafuatilia watoto wao wakiwa shuleni na wanafunzi kutojali
nini kilichowapeleka shule.
Wakiweka maazimio ya pamoja juu ya nini kifanyike
kukabiliana na hali hii, wamesema kuwa serikali kuu lazima isikilize kilio cha
walimu na iache kutumia nguvu na vitisho pale wanapodai haki zao za msingi, hii
ikiwa ni pamoja na kuboresha miundombinu
kama vile vitabu vilivyo na ubora, maabara, madarasa na walimu wenye sifa zinazokidhi
mahitaji ili kuzalisha watalaam bora nchini.
Kwa upande wa Halmashauri ya wilaya ya Karagwe,
wadau hao wameshauri kukamilisha ujenzi
wa chuo cha ualimu cha Ihanda ,kuharakisha
uanzishwaji wa kidato cha tano na sita na vyuo mbali mbali mbadala vya kuwawezesha
wanafunzi kuendelea na masomo ya stadi za maisha na ufundi za kuweza kujiajiri
kwa maisha yao yabadae.
Mdahalo huu umewahusisha mashirika mbalimbali yasiyo ya
kiserikali, walimu, wazazi na wanafunzi waliomaliza kidato cha nne mwaka 2012
zaidi ya 100 wakiwemo Mkrugenzi wa Radio fadeco, Mwenyekiti wa Kikosi kazi cha elimu wilayani
Karagwe ambaye pia ni Katibu Mkuu wa
shirika la KARADEA, na wawakilishi wa wazazi.
No comments:
Post a Comment