Mbunge
wa Musoma Vijijini
ambaye pia ni
Waziri wa Nishati
na Madini Profesa Sospter Muhongo
amepiga marufuku vikao
vyote vya baraza
la madini wa
halmashauri ya Musoma
Vijijini Kufanyika Manispaa
ya Musoma na
badala yake shughuli
zote za halmashauri
hiyo zifanyike eneo
la Mulangi ambako
ndiko kunatarajiwa kujengwa
makao makuu ya
wilaya.
Agizo hilo
amelitoa kwenye kikao cha
kujadili mambo ya
uchumi na maendeleo
ya jimbo hilo kilichofanyika eneo
la Mulangi ambapo
amesema kuwa ili
kusogeza huduma kwa
karibu na wananchi
kuna kila sababu
vikao na shughuli
zote zinazohusu halmashauri
hiyo kufanyika eneo
hilo ili ikue haraka.
No comments:
Post a Comment