Mbunge wa jimbo la Kawe jijini Dar es Salaama kupitia Chama cha demokrasia na Maendeleo (CHADEMA)HALIMA MDEE amembwaga mahakamani aliyekuwa mgombea wa kiti hicho katika uchaguzi mkuu 2015 kupitia CCM KIPPI WARIOBA katika kesi ya kupinga matokeo ya uchaguzi huo ambao HALIMA MDEE alitangazwa mshindi.
Mbunge huyo ameibuka mshindi baada ya kumwekea WARIOBA pingamizi kupitia kwa wakili wake Peter Kibatara kuwa kesi hiyo ilikuwa na dosari za kisheria ikiwa ni pamoja na kutotaja kifungu cha sheria alichotumia kufungua kesi hiyo.
Kutokana na hoja hizo wakili wa KIPPI WARIOBA EMMANUELI MAKENE alikubaliana na pingamizi hilo na kuomba kuiondoa kesi hiyo mahakamani.
No comments:
Post a Comment