Thursday, May 10, 2012

HII NI BAJETI YA KARAGWE

Na: Mbeki Mbeki

Halmashauri ya wilaya ya karagwe Mkoani Kagera imepitisha bajeti ya shilingi zaidi billioni 49, itakayotumika katika kipindi cha mwaka 2012/2012 zitakazo tumika katika matumizi mbalimbali ya Halmashauri hiyo.

Hayo yalisemwa jana na kaimu Mkurugenzi  Mtendaji wa Halmashauri Ernest Mwinga Kahabi wakati akisoma makisio ya bajeti katika kikao cha baraza la madiwani kilichofanyika kwa muda kwa siku mbili katika ukumbi wa Angaza uliopo mjini Kayanga Wilayani humo.

Kahabi alisema kuwa Halmashauri yake inategemea kupata jumla ya shilingi Billioni  49,184,627, 455.00 ambazo zitatumika katika kipindi cha mwaka 2012. Hadi 2013. Katika matumizi mbalimbali ikiwemo mishahara miradi ya maendeleo na matumizi mengineyo kwa idara zilizopata ruzuku.

Alisema kuwa kati ya fedha hizo kiasi cha shilingi 18,052,882 ni kwa ajili ya utekelezaji wa miradi ya maendeleo na kuwa mapato ya ndani yamekisiwa kuwa ni shilingi 3,887,446,400.00  na aliongeza kuwa kiasi cha shilingi 27,244,776,173 kuwa ni kwa ajili ya mishahara na matumizi mengineyo.
Aliongeza kuwa katia ya fedha hizo kiasi cha shilingi 22,971,413,280.00 ni kwa ajili ya watumishi na kaisi cha shilingi ni 4,273,362,893.00 ni kwa ajili ya shughuli za uendeshaji wa ofisi.

Kahabi alisema kuwa mapendekezo ya bajeti na mpango wa maendeleo na mwaka 2012 hadi 2013 yameandaliwa kwa kuzingatia sheria za serikali za mitaa na 7,8, na 9, za mwaka 1982 na kuwa ni kwa mujibu wa katiba ya nchi ibara ya 6,8,135 na 145.

Alieleza kuwa mapato ya Halmashauri hiyo yatatokana na ruzuku kutoka serikalini vizuizi vilivyo barabarani, ushuru wa mazao, mifugo na kutoka katika miradi mbalimbali ya maendeleo.

Aidha alisema kuwa mwongozo wa bajeti wa mwaka 2011/2012 ambao unaakisi maeneo 13 ya vipaumbele yaliamishwa na Rais Jakaya Mrisho Kikwete kwenye uzinduzi wa Bajeti mwaka 2010 kuwa maeneo hayo ya upaumbele yanaonesha  rasilimali za umma zinakopeshwa kuelekezwa ili kuchochea maendeleo na kushughulika matatizo ya nchi jamii na kiuchumi.

Hata hivyo baraza la madiwani wa Halamashauri  hiyo waliipitisha Bajeti hiyo na kushauri kuwa Bajeti hiyo itumike kwa makusudio yaliyo kusudiwa na kuonyesha  matumizi mabaya ya fedha za umma zinazotumika kwa manufaa ya wachache kuwa hawatavumilia watumishi wa aina hiyo.

No comments:

Post a Comment