NaMbeki Mbeki ,
TAASISI
ya kuzuia na kupambana na rushwa (TAKUKURU) mkoani kagera imekiri
kuelemewa na udhibiti wa kesi za rushwa kutokana na watu wengi kutotoa
ushirikiano kwa taasisi hiyo,mkanganyiko wa baadhi ya habari
zinazoripotiwa kwenye vyombo vya habari kuharibu mwenendo wa
upelelezi,pamoja na vitendo vya rushwa kufanyika kwa siri kubwa.
Akizungumza
kwenye mafunzo maalumu ya waandishi wa habari mkoani kagera (KPC)
Mwezeshaji wa taasisi hiyo Doreen Kapwani alisema rushwa kamwe haiwezi
kwisha katika jamii kwa kuwa ilikuwepo tangu enzi za mababu,huku
akitolea mfano wa dhambi kuendelea kutendeka licha ya viongozi wa dini
kukemea hali hiyo kila mara.
Kufuatia
hali hiyo alisema Taasisi hiyo imelazimika kutoa mafunzo maalumu kwa
waandishi wa habari ili kuwajengea uwezo wa kuandika habari za kufichua
vitendo vya rushwa hasa vijijini kwa lengo la kudhibiti ubadhilifu wa
fedha za miradi ya Umma,taasisi na watu binafsi.
Alisema
vyombo vya habari ni nguzo muhimu sana katika kupambana na vitendo vya
rushwa katika jamii na kwamba taasisi hiyo imeamua kufufua mahusiano
mapya na waandishi wa habari nchini baada ya kuwepo ukimya wa vyombo vya
habari kuripoti habari zinazohusu rushwa.
Kwa
mujibu wa mkuu wa wilaya ya Bukoba Samwel Kamote ambaye pia alikuwa
mgeni rasmi katika uzinduzi wa mafunzo ya siku tatu yaliyoanza
jana,viongozi wote wa serikali wanatakiwa kuwa wazi kwa waandishi wa
habari katika kueleza mambo ambayo wangependa kupata ufafanuzi badala ya
kuficha habari hizo ambazo ni mhimu kwa jamii.
Kamote
alisema kushindwa kutoa ushirikiano kwa waandishi wa habari ni kujenga
tabaka bovu ambalo linaweza kusababisha uvunjifu wa amani kwa
jamii,baada ya kuandikwa habari ambazo hazina usahihi.
Kuna
haja kubwa kwa vyombo vya habari nchini kujikita zaidi katika kuandika
habari za vitendo vya rushwa kwa kuwa visipo ibuliwa vinaweza kuendelea
kuathiri zaidi wananchi maskini,hivyo kupelekea kukosa imani na serikali yao.
Alidai
kuwa waandishi wa habari wanatakiwa kuwa na ushirikiano mkubwa na
taasisi ya kuzuia na kupambana na rushwa badala ya kuweka daraja dhidi
yao hali ambayo inaweza kusaidia kupunguza vitendo vya kutoa na kupkea
rushwa.
No comments:
Post a Comment