Tuesday, May 22, 2012

HUU NI KUTOKUWA NA UCHUNGU WA KUINUA UCHUMI WA KARAGWE

Na: Mbeki Mbeki
Baraza la madiwani la Halmashauri ya Wilaya ya Karagwe limekataa kupitisha mradi wa kitega uchumi chenye thamani ya shilingi billion 50, kutokana na kuhusishwa  na vitendo vya rushwa.
Chanzo cha habari hizi kimeeleza kuwa madiwani wote bila kujali itikadi zao za vyama wameukataa mradi huo, ambao wamedai umeghubikwa na harufu ya ufisadi ambapo walieleza kuwa kitega uchumi hicho kilikuwa  kijengwe kwa kukopwa na benki ya ADB kwa kushirikiana na NSSF.
 
Madiwani hao ambao hawakuwa tayari kutaja majina yao katika vyombo vya habari walisema kuwa baada ya kikao cha kawaida cha baraza  la madiwani walikaa kama kamati kujadili ujenzi wa kutega uchumi ambacho walisema awali kilikuwa kimekadiriwa kugharimu jumla ya  shilingi Billioni 27,600,000/= kiasi ambacho kitatolewa na NSSF kama mkopo kwa halmashauri za Kyerwa na Karagwe. 
 
Chanzo cha habari hizi kilieleza kuwa madiwani hao waliamua kukataa kutokana na kwamba agenda hiyo ililetwa na mwenyekiti wa Halmashauri hiyo bila kufuata maazimio ya vikao na kuwa alishindwa kulieleza baraza lake ni kwa namna gani wataweza kulipa deni watakalo kuwa wamekopwa na kuwa ni nani atakayesimamia mradi huo katika hatua nyingine madiwa hao walieleza kuwa eneo lililokusudiwa kujenga kitega uchumi ni eneo lililokusudiwa kujenga kwa ajili ya stendi ya magari kuwa mchakato mzima wa ujenzi ulipaswa kuwashirkisha wananchi  ambao ndio wadau wa kubwa wa Halmashauri na maendeleo kwa ujumla. 
 
Pia chanzo cha habari hizi kilieleza kuwa eneo hilo lilishagawiwa kwa wananchi ambao walitaka kujenga vyumba vya kukodisha kwa ajili ya kuzunguka stendi ya magari, amabpo walisema nao walipaswa kushirikishwa, jambo ambalo walisema halikufanyika. 
 
“ Ninachoweza kukueleza bila uficho ni kwamba mwenyekiti wetu anataka kutuburuza kwa maslahi yake ukisoma kwenye kablasha letu uk.19 yaliyoandikwa ni uongo madiwani hatujakubaliana na mtu katika uejnzi wa kitega uchumi” Alisema.
 
Uchunguzi ulionyesha kuwa hata kamati ya fedha ya Halmashauri ilikataa shinikizo la mwenyekiti wa Halmashauri hiyo kutaka ujenzi huo uanze mara moja na kuwa baraza la madiwani lipitisha kiasi cha milioni 15 kwa ajili ya kuanza mchakato  wa ujenzi.
Aidha madiwani hao walikataa kuwahi  kufanya makubaliano ya kkujenga kitega uchumi cha stendi katika mji wa kayanga uliopo wilayani hapa na kuingia makubaliano na mashauri msanifu wa majengo wa kampuni ya CONS AFRICA LIMITED na kufadhiliwa na shirika la hifadhi ya jamii (NSSF). Hata hivyo madiwani hao walisema kuwa yapo makampuni na watu binafsi wanaoweza kuwajengea mradi kama huo wenye gharama zinazokopesheka kulingana na mapato ya Halmashauri yao. 
 
“ Huyu mwenyekiti anataka tushindwe kufanya kazi za maendeleo na tufikirie  kulipa madeni,  na hili litatupelekea kupiga kura ya kutokuwa na imani naye kwani theruthi mbili zikimkataa tunastisha uchaguzi tumechoka kuburuzwa” Alisema. 
 
Kwa upande wake  mwenyekiti wa Halmashauri hiyo kushunju runyogoote alipohojiwa kuhusiana na tuhuma zilizoelekezwa kwake alisema kuwa ameshindwa kuelewa kwanini madiwani wenzake wameamua kumgeuka na kupigana na maazimio waliyowahi kuyaazimia. 
 
Runyogote alikanusha kuwa hakuna miaya ya nushwa inayoenelekezwa katika ujenzi wa mradi huo bali ni suala zima la kuwatetea wananchi maendeleo. 
 
Aidha uchunguzi wa haabri hizi umeonyesha kuwa kikao cha dharula  cha baraza la madiwani wa Halmashauri hiyo kimeitishwa tena mei 23 mwaka huu katika hali ambayo imeelezwa kuwa ni katika mstakhabali wakunusuru kati cha mwenyekiti au kura ya kutokuwa na imani na nafasi akiyo nayo.

No comments:

Post a Comment