KARDINALI RUGAMBWA KUZIKWA
Askofu msaidizi wa jimbo katoliki la Bukoba, Methodius Kilaini akizungumza na waandishi wa habari kuhusu kuhamisha mwili wa Kardinali Laurean Rugambwa kutoka alikozikwa kwa muda katika kanisa katoliki la Kashozi na kuzikwa rasmi katika kanisa katoliki la jimbo kuu la Bukoba, ambako alichagua kuzikwa.
Na
Mwandishi wetu
Bukoba.
Kardinali
wa
kwanza Afrika na askofu wa kwanza Mwafrika Mwadhama Laurian Rugambwa
ambaye
alizikwa kwa muda katika kanisa la Kashozi mwaka 1997, hatimaye atazikwa
rasmi
katika kanisa kuu jimbo Katoliki la Bukoba, baada ya ukarabati wake
kukamilika.
Askofu
msaidizi
wa jimbo Katoliki la Bukoba Methodius Kilaini alisema kuwa maamuzi ya
marehemu Rugambwa kuzikwa Kashozi yalitokana na kanisa hilo alilochagua
kuzikwa
kuwa katika ukarabati tangu mwaka 1996.
Askofu
Kilaini
alisema kuwa mazishi hayo rasmi yatafanyika Oktoba 6 mwaka huu, siku
ambayo pia itakuwa ni kumbukumbu ya miaka 100 ya kuzaliwa kwa Kardinali
Rugambwa ambaye alizaliwa mwaka 1912.
“Masalia
ya Kardinali Rugambwa yatahamishwa rasmi siku
hiyo kutoka kanisa Katoliki la Kashozi, tutasherehekea miaka 100 ya
kuzaliwa
kwake, lakini pia siku hiyo Kanisa Katoliki jimbo la Bukoba
litatabalukiwa”
alisema.
Alisema
kitendo
hicho ni kumbukumbu nzuri kwa
Watanzania na Waafrika kwa ujumla kutokana na kuwa Kardinali kwa kwanza
Afrika
na Askofu wa kwanza Mwafrika, hivyo wanategemea kupata wageni wengi
kutoka ndani
na nje ya nchi.
Kuhusu
mgeni
rasmi atakayealikwa siku hiyo alisema atajulikana baada ya kikao cha
maaskofu ambao wanatarajiwa kukutana mwezi Juni mwaka huu, ambapo pamoja
na
mambo mengine watapanga na kukubaliana nani atakuwa mgeni rasmi.
Alisema
kuwa
baada ya shughuli hizo, kanisa Katoliki jimbo la Bukoba linataendelea
kutumika kwa ibada za kawaida, na kuwaondolea waamini wao adha ya
kusalia
katika holi.
“Tunaendelea
kuhamasisha
waamini wetu wachangie fedha kwa ajili ya kumalizia sehemu ya
ujenzi iliyobaki, lakini pia wachangie sherehe hizo ili ziweze kufanyika
kwa
ufanisi” alisema Askofu Kilaini.
Akizungumzia
historia
ya Kardinali Rugambwa alisema kuwa alipewa Upadre mwaka 1943, mwaka
1952 akapewa Uaskofu, mwaka 1960 akawa
Kardinali na mwaka 1969 akawa Askofu Mkuu Dar-Es-Salaam hadi
alipostaafu mwaka 1992.
Akigusia
kidogo
aliyoyafanya Kardinali Rugambwa ambayo baadhi yake yanawafanya watu
waweze kumkumbuka, Askofu Kilaini alisema kuwa alianzisha kanisa kuu
jimbo la
Bukoba, alileta seminari kuu ya Ntungamo na alijenga shule ya sekondari
Rugambwa.
Mengine
ni
ujenzi wa hospitali ya Mugana, kuanzisha vikoba kwenye parokia,
kuanzisha
seminari ndogo ya Visiga na kuanzisha seminari kuu ya Segerea zilizoko
Dar-es-Salaam.
No comments:
Post a Comment