Na Mbeki Mbeki
MVUA ZIMEATHILI MIUNDOMBINU YA BARABARA KARAGWE.
Mvua zinazoendelea kunyesha katika Wilaya ya Karagwe
Mkoani Kagera imeleta madhara makubwa ya
kuharibu miundombinu ya barabara, ikiwemo mazao ya kilimo.
Akizungumza jana na waandishi wa habari Diwani wa Kata ya
Kihanga Josephat Kibate alisema kuwa barabara kuu kutoka mjini Kayanga kuelekea
Bukoba mjini imefungwa kwa muda kutokana na kukatika kwa daraja na mafuriko
makubwa yaliyopelekea barabara hiyo kuharibika kabisa
Kibate alisema kuwa mvua zinazoendelea kunyesha tangu April,
30 mwaka huu zimeleta maadhara makubwa ya kuharibu miundo mbinu ya barabara ni
pamoja na kuharibika kwa mazao ya kilimo.
Alisema kuwa mvua hizo zimekata mawasiliano kati ya Kata na
Kata na Wilaya na Wilaya ambapo alisema kuwa kwa muda wa siku tatu magari yote
ya abiria hayakuweza kusafiri na
wananchi walishindwa kufanya shughuli zao za maendeleo.
Aliongeza kuwa zaidi ya hekari 50 za maharage katika Kata
yake zimeharibiwa na mvua ni pamoja na na kahawa ambayo kwa kipindi hiki
alisema mvua zinapoendelea kunyesha zao hilo uharibika na kuharibu uchumi wa
Wilaya na Taifa.
Kwa upande wake, Diwani kwa Kata ya Kibondo Jean Adamu
alisema kuwa barabara inayotoka Katani kwake yenye urefu wa km 30 kuelekea
Makao makuu ya Wilaya imeharibika sana
ambapo aliongeza kuwa magari makubwa ya wafanya biashara yamekwama katika
barabara hiyo kutokana na mafuriko.
Alisema kuwa barabara hiyo imekuwa korofi kwa muda mrefu
kutokana na kujengwa chini ya kiwango, na kuwa nyakati za mvua abiria wamekuwa
wakipata usumbufu kutokana na maji mengi kutuama barabarani.
Aidha mkuu wa Wilaya ya Misenyi Kanali Mstaafu Issa Njiku
akizungumza na gazeti hili kwa njia ya simu kutoka Dodoma alikiri Kuwepo kwa hali hii ya
mafuriko katika sehemu mbalimbali za Wilaya yake na wananchi wengi kuathirika
kutokana na mafuriko ya mvua.
Hata hivyo amewataka wananchi Wilayani humo wanaoishi katika
mabonde kuhama mara moja katika maeneo hayo kuwa hategemei kusikia lawama
baadae zikielekezwa kwa Serikali kutokana na Ofisi yake kutoagiza hilo kwa wananchi.
“ Nimekuwa mara kwa mara nawaagiza wananchi kuepuka kujenga
mabondeni lakini baadhi ya wananchi ni wagumu kutekeleza maagizo hayo madhara
yake wameathiriwa na mafuriko” Alisema Njiku.

No comments:
Post a Comment