Na:
Mbeki Mbeki
Baada ya vitendo vya ubakaji
kupungua kwa watoto waliochini ya Umri, vimezuka vitendo vya ulawiti kwa watoto
wadogo katika Halmashauri ya wilaya ya Karagwe
Mkoani Kagera.
Hayo yalisemwa jana na Kaimu Mkuu wa wilaya hiyo Kanali
Msttaafu Sulemani Issa Njiku ambaye pia ni Mkuu wa wilaya ya Misenyi wakati
alipokuwa akizungumza na waandishi wa habari ofisini kwake wailayani humo.
Kanali Mstaafu Njiku alisema
kuwa baada ya vitendo vya ubakaji kupungua kwa watoto walio dhini ya umri na kukithiri kuwa sasa kumezuka vitendo vya
ulawiti kwa watoto wadogo katika wilaya hiyo na kuripotiwa ofisini kwake.
Alisema kuwa vitendo hivi
vya aibu ni ukikukaji wa haki za binadamu, kuwa anasikitika kuona kuwa wazazi
wengine wanahusika kuwalawiti hata
watoto wao wakuzaa.
“ Mzee mwenye umri wa miaka
54 ameletwa ofisini kwangu hapa Karagwe kwa kosa la kumlawiti mtoto mdogo wa
miaka 10, polisi wakikamilisha kazi yao tutampeleka mahakamani huu si unyama kweli” Alisema Njiku.
Alisema kuwa vitendo hivi
vinavyosababishwa wa baadhi ya vijana wanaokunywa madawa ya kulevya ni pamoja na unywaji wa vinywaji
vikali ikiwemo uvutaji wa bangi ambao alisema
hata katika wilaya hiyo umekithiri.
Aidha aliongeza kuwa mkakati
uliotumiwa na kamati ya ulinzi usalama katika wilaya hiyo kwa kuhakikisha
vitendo vya ubakaji na mimba za utotoni zina pungua hata vitendo hivi vichafu
vitakomeshwa ambapo pia kuwa watawashirikisha wananchi wema
kuwafichua watu hao wabaya.
Hata hivyo amewataka wazazi
katika wilaya hiyo kuka a karibu na watoto wao kwa muda wote na kuwasaidia katika malezi mamea na kuacha
tabia ya kuwatuma kwenye vilabu vya
pombe na majira ya usiku.
No comments:
Post a Comment