Thursday, May 10, 2012

TUWAUNGE MKONO KUOKOA JAHAZI HILI

Jumla ya shilingi Billioni 500 zinahitajika  kukamilisha ujenzi shule ya watoto walemavu walipo katika  halmashauri ya wilaya ya karagwe mkoani kagera. 

Kauli hiyo ilitolewa jana na sisita  Godeliva Mboyerwa kutoka jimbo la kikatoriki ka kayanga katika semina iliyowahusisha  walemavu 42, iliyofanyika katika ukumbi wa Angaza wa halmashauri hiyo iliyopo mjini Kayanga.

Sista mboyerwa alisema kuwa jumla ya shilingi billioni  500 zinahitajika kukamilisha ujenzi wa shule ya msingi mwoteka center inayoendelea kujengwa kata ya Nyabiyonza, kijiji cha Chabalisa na kanisa katoriki kwa kushirikiana na Halmashauri ya wialya ya karagwe.

Alisema kuwa shule hiyo ya walemavu inajengwa kwa madhumuni ya kukuza na kuimalisha vipaji vyao kuwapunguzia mazingira hatarishi, kuwapa  upendo katika kuwahudumia kuwa ni pamoja  na kuwafanya kuwa sawa na watoto wengine wasio na ulemavu katika mahitaji ya kielimu, ambapo aliongezea kuwa madarasa  mawili yameisha kamilika na kuwa shule hiyo itakuwa ya bweni ambayo haitakuwa na itikadi yadini yoyote.

Sista Mboyerwa alisema kuwa wanacnhi waondokane na dhana potofu  ya kuwanyanyapaa walemavu na kuwa walemavu wanayo haki sawa na watu wengine kuwa wananchi wanapaswa kuchangia ujenzi wa shule hiyo inayoendelea kuejngwa. Kwa  upande wake  mwenyekiti wa Halmashauri ya wilaya  hiyo Kashunju Runyogote alisema kuwa katika ujenzi wa madarasa Halmashauri imechangia shilingi milioni 25, ujenzi wa bweni shilingi milioni 74, na kuongezea kuwa katika mwaka wa fedha 2012 hadi 2013, zimetenhwa shilingi milioni 120 kwa ajili ya kukamilisha ujenzi wa shule ya walemavu. 

Aidha alisema kuwa halmashauri hiyo imetenga shilingi milioni 95. Kwa ajili ya kuwalipia wanafunzi wenye ulemavu wa ngazi karo  wanasoma katika shule ya walemavu iliyopo  Kitengure Mkoani Kagera.
Hata hivyo, amewataka viongozi wa vijiji na kata kuwaorodhesha watoto wote wenye ulemavu wa aina yoyote ili shule itakapofunguliwa waweze kusajiliwa na kuanza masomo na kuongezea kuwa walimu watakaofundisha katika shule hiyo watakuwa ni wenye elimu maalum na kuwa Halmashauri hiyo kwa kushirikiana na Kanisa wanakusudia  kuifanya shule ya mchepuo wa kiingereza.

No comments:

Post a Comment