Saturday, June 16, 2012

HAYA WANAOPENDA MCHEZO WA SIASA TUNAJUA SIASA NI SEHEMU YA MAISHA ILA KINACHOTENDEKA MMM NA WAACHIA WENYEWE

NA MBEKI MBEKI

Vyama vya siasa vya upinzani katika Wilaya ya Karagwe Mkoani Kagera vimetishia kumfikisha Mahakamani, Mwenyekiti wa Halmashauri hiyo kutokana na tuhuma mbalimbali ikiweno matumizi mabaya ya madaraka.
 
     Madiwani wa vyama vya siasa vya upinzani wakizungumza jana na waandishi wa habari  walisema kuwa wanakusudia kumfikisha mahakamani Mwenyekiti wa Halmashauri hiyo Kashunju Runyogote ktokana na tuhuma mbalimbali ikiwemo matumizi ya mabaya ya madaraka.
 
     Madiwani hao kutoka vyama vya siasa vya CHADEMA, CUF, na TLP walizitaja baadhi ya tuhuma nyingine kuwa ni kutumia vibaya gari la Halmashauri na kujipatia mafuta kinyume cha utaratibu, kubadili maazimio ya vikao vya baraza la Madiwani kwa maslahi yake, na kufanya shughuli za Halmashauri bila kushirikisha Baraza la Madiwani.
 
     “Lazima tumpeleke pabaya Halmashauri ameigeuza mali yake anataka atuburuze
      anavyotaka tumechoka na ufisadi anaoufanya” Walisema.
 
     Walisema kuwa kwa ushirikiano wa vyama vyote kikiwemo chama tawala chama cha mapinduzi (CCM), walisha kusanya sahihi (31) za kutokuwa na imani na Mwenyekiti huyo, kuwa Juni 7 mwaka huu Madiwani wa chama cha mapinduzi (CCM, walioweka sahihi zao nakutishiwa kupelekwa katika kamati ya maadili na kubadili msimamo wao.
 
          “Viongozi wa CCM ngazi ya Mkoa, kwa kushirikiana na Katibu wa CCM Wilaya walijitoa kumnusuru mwenyekiti huyo kwa kuwatisha Madiwani wao lakini kwa kuwa tulishipata sahihi zao tutaendeleza mapambano” walieleza.
 
     Walisema kuwa uamuzi wa kumng’oa Mwenyekiti huyo ulitolewa katika kikao cha Madiwani wa Halmashauri hiyo Mei 8 mwaka huu baada ya Madiwani 22 kati 42 wa CCM kuwasilisha hati ya kutoa tamko la kutokuwa na imani naye kwenye kikao cha Baraza lao, na  Madiwani tisa kutoka vyama vya upinzani.
 
     Aidha wamewataka Madiwani wenzao kutanguliza maslahi ya wananchi kuliko kutanguliza itikadi za vyama vyao.
 
          “Hapa walichokifanya nisawa na zero, kwani wamemnusuru mtu hawakunusuru chama hizi hoja lazima tuzipeleke kwa wananchi, na majukwaami, hatuwezi kukubali kodi ya walipakodi kuliwa na mtu mmoja kwa kisingizio cha kulinda. Ilani za kifisadi” walisema.
 

No comments:

Post a Comment