Saturday, June 16, 2012

KILA CHENYE FAIDA LAZIMA KUWEPO NA HASARA.

Na:- Mbeki Mbeki

     Watu sita wamefariki dunia kwa kupigwa na radi katika kata ya Kibingo Wilaya Kyerwa, Mkoani Kagera.

     Kamanda wa Polisi wa Mkoa wa Kagera Bw. Phillip Kalangi aliwataja walio pigwa na radi na kufariki hapo hapo baada ya kupigwa na radi kuwa ni Methodia Kaledunia (35), Bateganya Kamashana miezi 10, Kamugisha Kamashara miaka 2 na miezi 4, Kazungu Emmanuel miaka (15) mwanafunzi wa darasa sita Shule ya Msingi Kihinda, Dawson Aaron (16) mwanafunzi wa darasa la sabashule ya msingi Kihinda na Revelian Wilison umri wa miaka mine.

     Tukio hilo lilitokea Juni 8 majira ya jioni katika Kijiji cha Kihinda, Wilayani Kyerwa, ambapo alisema kuwa watu hao walipigwa na radi wakati wakiwa wamejikinga na mvua kwa jirani yao , na kati ya watu hao watatu walikuwa wanatoka katika familia moja.

     Alisema katika tukio hilo mbuzi watano walikufa hapo hapo kwa kupigwa na radi, nyumba moja na baadhi ya mashamba ya wakulima yaliharibiwa vibaya na radi.

     Kwa mujibu wa maelezo ya mtendaji hiyo Jofry Milambwe alisema kuwa watu watatu wafamilia moja wamezikwa katika kaburi moja kutokana na mwili yao kuharibika vibaya ambapo aliongeza kuwa Tukio la radi katika Kata hiyo ni latatu ambapo alisema kuwa kati ya mwaka 2007 na 2010 ng’ombe kadhaa walipigwa na radi na mashamba kadhaa.

     Jeshi la Polisi Wilayani hapa linaendelea kufuatilia taarifa za uharibifu wa sehemu mbalimbali kutokana na mvua zilizonyesha na kuleta madhara makubwa

No comments:

Post a Comment