Madereva wa vyombo vya usafiri wilayani Ngara wataka mikataba ya kazi toka kwa waajiri wao
Madereva wa vyombo vya usafiri walioko wilaya ya Ngara mkoani Kagera wamewataka wamiliki wa vyombo hivyo kuwapa mikataba ya kazi ikiwemo mishahara kwa mwezi pamoja na kupunguza kiwango cha mawasilisho ya fedha kwa siku ili wafanye kazi zao kwa kuzingatia sheria za usalama barabarani
Mmoja wa Madereva mjini Ngara Medard Mpanju alitoa kauli hiyo Julai 28 katika kikao cha wamiliki wa vyombo vya usafiri , madereva na kikosi cha usalama barabarani kilichoongozwa na mkuu wa Wilaya ya Ngara Bw Costantine Kanyasu kwenye ukumbi wa Paradise mjini Ngara
Mpanju alisema kuwa maderva wanafanya kazi katika mazingira magumu kwa kulazimika kubeba abiria wengi katika chombo cha usafiri ili kuwasilisha mapato kwa tajiri kati ya shilingi elfu 30 hadi elfu 40 kwa siku na hatimaye kujikuta wakivunja sheria kwa kubeba abiria kupita kiasi ukiwemo mwendo kasi katika vituo vyote wilayani humo
Wakati huo huo madreva wa pikipiki wanaofanya kazi ya kubeba abiria katika wilaya hiyo walisema wanafanya kazi katika
mazingira magumu kutokana na changamoto ya kukosa leseni kutoka makao makuu ya wanafanya kazi katika mazingira magumu kutokana na changamoto ya kukosa leseni kutoka makao makuu ya mkoa ambapo kazi yao inakuwa ngumu kwa kukimbizana na jeshi lapolisi hasa askari wa usalama barabarani kwa kuwa hufanya kazi kwa kuvunja sheria na kusababisha kuwepo mianya ya rushwa kwa askari wasio waadilifu kwenye kazi yao
Mwenyekiti wa madereva hao Yazzidu Wilsoni Masha alisema kwa sasa wamejiunga katika vikundi vya kukopeshana kupata mafunzo na leseni lakini kero kubwa ni kupata leseni toka makao makuu ya mkoa ambapo ni mbali na wilaya hiyo wanakofanyia kazi zao za kusafirisha abiria
“Tumeanza kuunda umoja wa kuchangiana kupata leseni kwa kila mmoja kuchangia shilingi elfu 60 kila mwezi na kulipia shilingi elfu tano kila siku ili baadaye kupata shilingi milioni mbili ili kuwa na chombo binafsi kwa lengo la kujiajiri” AlisemaWilson Masha
Alisema pia serikali kupitia tanroard iweke ishara za alama za usalama barabarani na halmashauri wilayani humo kuweka miundombinu rafiki kwenye standi za magari katika vituo vya Ngara mjini ,Kabanga ,Rulenge na Benaco kwa kuwa magari yanayoingia katika vituo hivyo hulipia ushuru kama vyanzo vya mapato
Hata hivyo mkuu wa jeshi la polisi wilayani Ngara Mohamed Milanzi alisema jeshi la polisi wilayani humo litahakikisha sheria zinafuatwa na kuondoa changamoto zilizopo kwa wamiliki wa magari pikipiki wakiwemo madereva wa vyombo hivyo likiweo na jeshi lenyewe .
Milanzi aliwataka askari wa usalama barabarani wanaokiuka maadili ya kazi zao kuhakikisha wanatambua miiko ya kazi kwa kuepuka rushwa uonevu na vitisho au kujichukulia sheria mkononi na kuhatarisha usalama kwa raia na mali zao jambo la msingi ni kuhamasisha jamii kutii sheria bila kushurutishwa.
Katika hatua nyingine Mkuu wa wilaya ya Ngara Bw Costantine Kanyansu aliwataka wamilikina waendesha vyombo vya usafiri kufanya kazi kwa kuzingatia sheria za usalama barabarani ili kupunguza ajali zisizo za lazima na kuendelea kuhatarisha maisha ya watu huku serikali ikipoteza watu ambao ndio wanaotegemewa katika kukuza uchumi na kuleta maendeleo ya Taifa
Kanyasu alisema ili chombo kiweze kufanya kazi barabarani ni bora kisiwe na hitilafu, sambamba na kufuata taratibu za kupakia abiria na mizigo ili kuhakikisha chombo kinakuwa katika hali ya usalama pamoja na abiria huku wakiepuka mwendo kasi ambao hushindwa kusoma hata alama za Tan Roard zilizopo kwenye maeneo wanakopita .
Aidha alitoa muda wa miezi miwili kwa maderva wa vyombo vya usafiri wasio na leseni kuhakikisha wanazitafuta na kuzisajili ili kufanya kazi kwa kuzingatia sheria na jeshi la polisi lifanye utaratibu wa kuwahamasisha watoa leseni mkoani kufika wilayani Ngara kuwakatia leseni hizo pamoja na mafunzo ya sheria ili kurahisisha kazi zao.
Mkutano huo ulifanyika baada ya kuwepo migogoro kari ya madereva na jeshi la polisi miezi miwili iliyopita ambapo askari mmoja alimpiga dereva kwa kukiuka sheria ya kujaza abiria wengi na kumsababishia maumivu na kulazwa katika Hospitali ya Nyamiaga wilayani humo na askari waliohusika kesi yao inasikilizwa katika mahakama ya kijeshi mkoani Kagera
Ikiwa ni hatua ya kutafuta ufumbuzi wamatukio ya ajali za barabarani zinazo tokea mara kwa mara wilayani Ngara mkutano huo ulihusisha pande zote mbili serikali na vyombo vyake vya dola vinavyosimamia sheria na wamiliki wa vyombo vya usafiri pamoja na watumiaji wa kila siku wa vyombo hivyo ambavyo huingia barabarani huku vikiwa na lengo la kumsaidia mjasilia mali kupambana na umaskini hapa nchini.
No comments:
Post a Comment