Friday, August 3, 2012

TUWAJIBIKE KWA NAFSI ZETU KULETA UFANISI WA MAENDELEO

DC NGARA AWATAKA  WATENDAJI KUSIMAMIA MAENDELEO YA WANANCHI
Watendaji wa  idara za serikali  na taasisi  za umma  wametakiwak uwajibika ipasavyo  katika kuleta maendeleo ya wananchi  kwa kuzingatia sheria  taratibu na kanuni za kazi zao bila kusumbuliwa  au kutishiwa na  viongozi wa vyama vya siasa kwenye maeneo yao.
Mkuu wa wilaya ya Ngara mkoani Kagera   Costantine Kanyasu alitoa kauli hiyo  julai 20 katika tarafa za Rulenge na Murusagamba wilayani humo wakati wa ziara yake ya kujitambulisha kwa viongozi na wataalamu mbalimbali wakiwemo Viongozi wa dini pamoja na wawakilishi wa vyama vya siasa katika tarafa hizo
Kanyasu alisema kuwa Viongozi wa serikali wawajibike kuleta maendeleo ya wananchi kwa kusimamia sera  na sheria za taifa na kuondoa umaskini katika mazingira wanakoongoza  jamii kwa kuangalia vipaumbele muhimu katika mahitaji ya jamii kwenye eneo husika. Alisema watendaji hao wasifanye kazi kwa kushambulia chama tawala kutokana na changamoto zilizoko katika jamii kwani chama hicho ndicho kilichoiweka serikali madarakani wanayoitumikia na kufanya hivyo ni kukiuka miiko ya utumishi na kuvunja sharia za kazi zao
Alisema kila mtendaji wa serikali kila ngazi ana mamlaka ya kuhakikisha anakuwa na  vipaumbele katika kukukuza kipato cha mwananchi kwa kuzalisha mazao ya kilimo  kibiashara kwa mkazi wa ngara  ili kuinua kiwango cha uchumi na kupunguza umaskini. Alisema kuwa katika mikakati yake akiwa wilayani Ngara ni kuongeza kiwango cha ufaulu wa  elimu ikiwa ni pamoja kukuza uchumi  wa mwananchi wa wilaya hiyo kisha kuimarisha  ulinzi na usalama kwa kuhakikisha wahamiaji haramu wanaondolewa kwa kufuata sheria za nchi
Alisema kipato cha mkazi wa wilaya hiyo ni dola 250 kwa mwaka na wananchi wanakuwa maskini kwa kukosa fursa za usimamizi mzuri wa kiutendaji kwa kuwa wanayo ardhi ya kutosha yenye rutuba ni jukumu la halmashauri ya kilimo kwa wakulima na wafugaji kwa kutumia zana bora za uzalishaji mali na kuongeza kiwango cha mazao na kutumika kuinua uchumi kwa kutumia fursa za mipaka baina ya wilaya hiyo nan chi za Rwanda na Burundi katika soko la Afrika ya mashariki
 
Aliwashauri viongozi hao wakiwemo wawakilishi wa vyama vya siasa na madhehebu ya dini kuweka kipaumbele kingine cha kuwapeleka watoto shule kupata wataalamu borawa  ndani na njeya nchi ili kuingia katika soko la ajira duniani ambao wataboresha maisha na uchumi wataifa.
Alisema viongozi wazazi na walezi wanaokwamisha juhudi za serikali kwa kuwaoza wanafunzi au kuwasababishia ujauzito na kushindwa kuwapa mahitaji ya elimu wanafunzi wa jinsia zote watakamatwa na kufikishwa kwenye vyombo vya dola kwani wilaya ya ngara inaasilimia 30 ya  wanafunzi ambao wameshindwa kuanza kidato cha kwanza kwa kukosa mahijata ya kielimu
Katika hatua nyingine Kanyasu alisema wilaya ya Ngara iko mpakani na nchi za jirani hivyo wananchi wasiwe na  huruma wa kuwakaribisha wageni na kuwahifadhi kwa kuwapa ardhi kupitia Nyanja za rushwa kwani wakisha kaa na kupata elimu kisha kuingia katika vyombo vya dola na kufanya kazi watawatumikisha watanzania kwa kuwafanya vibarua ndani ya nchi yao. Alisema kila mwananchi awe na machungu nan chi yake kwa kuonesha uzalendo na kutii sharia za nchi huku wakitoa taarifa sahihi za watu wanaokiuka taratibu za kuingia nchini bila vibali na kuwataja wale wanaowakaribisha ili waweze kuchukuliwa hatua za kisheria
Naye Diwani wa kata ya Bugarama wilayani humo Adroniz Bulindoli alisema serikali haina budi kuwondoa wahamiaji haramu walioko katika vijiji kwa kutumia vyombo vya dola kwani kuendelea kukaa wataharibu takwimu za nchi wakati wa sense ya watu na makazi katika kuweka na kusimamia mipango ya maendeleo nchini. Bulindoli alisema kuwa wapo baadhi ya wananchi wanaowakodisha mashamba na kugawana mazao wakati wa mavuno lakini wakati wa zoezi la kilimo wahamiaji hao hukaribisha ndugu zao na klatika mahusiano wapo wanaonunua mashamba na kuyamiliki kasha kuanzisha makazi ambapo siku za usoni watakuwa watawala katika serikali za vijiji kwenye vizazi vijavyo
Hata hivyo mkuu wa wilaya hiyo Costantine Kanyasu katika kusikiliza hoja za viongozi na maoni yao aliwasisitiza kufanya shughuli za maendeleo kwa kuweka pembeni tofauti zao za kiitikadi aidha za dini au siasa bali washikamane kuondoa changamoto zilizoko katika maeneo yao Alisema endapo kila mmoja atajua wajibu wake na mipaka ya majukumu kiutendaji  na   wilaya ya ngara kwa muda mfupi itabadilika kiuchumi  kielimu na kisiasa kwa kuzingatia fursa za ardhi madini ya Nickeli yanayotarajiwa kuchimbwa hivi karibuni wilayani humo na masoko katika afrika ya Mashariki

No comments:

Post a Comment